Tunapenda kutoa taarifa kwa Umma wa DMV kuwa, Team Libe for DMV Community President 2014 hatutambui uongozi mpya ulio tangazwa na Tume ya Uchaguzi jana August 11, 2014.   Msimamo wetu ni kuwa; tunapinga matokeo ya uchaguzi ulio fanyika August 9, 2014 kwani ulikuwa sio wa haki na ni BATILI.  

“Team Libe for DMV Community President 2014” haitatoa ushirikiano wowote na uongozi wa Jumuia ya Association of Tanzania Community in DMV.  Pia tunawaasa wale wapenzi wetu kuto kutoa ushirikiano wowote na uongozi huu batili hadi pale madai yetu yatakapo sikilizwa na kutatuliwa.  Tunaomba wapenzi wetu ambao walijitokeza kupiga kura wawe wavumilivu na watulivu katika kipindi hiki kigumu cha kunyang’anywa haki yao ya kimsingi ya kumchagua kiongozei wanao mtaka.  

Mwisho, “Team Libe for DMV Community President 2014” inaitaka “Board of Directors” kutengua uongozi huu uliopatikana kwa njia ya dhulma.  Ieleweke kuwa, Team Libe for DMV Community President 2014” na wafuasi wake hatutatoa ushirikiano wowote na uongozi wote wa jumuia.

Fuata hii link kusoma maelezo juu ya ubatili ya huu uchaguzi;


Imetolewa August 12, 2014
Team Libe for DMV Community President 2014

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Tokeni zenu Mnatuzingua
    Kwani lazima wewe ushinde ndio uchaguzi uwe halali?

    Nimekuwa nikifatilia sakata lenu toka mwanzo na ninapenda kukuambia kuwa

    Huo ni ushamba na wewe huwezi kuwa kiongozi kwani toka mwanzo ulilionyesha hilo na mtu yeyote makini asingeweza kukupa wewe kura yake

    Hassan
    Dar es salaam
    Tanzania

    ReplyDelete
  2. Kijana unaonyesha jinsi gani usivyo na sifa za kuwa kiongozi maana ulibebwa sana huu Uchaguzi lakini wana DMV majority wamemchagua kiongozi anaowafaa. Hekima na busara ni moja ya sifa kuu kwa kiongozi bora na hapa kama ni scale ya 0-10,basi utapata 0.

    ReplyDelete
  3. du.. ukishindwa kubali matokeo

    ReplyDelete
  4. Tangu lini uongozi wa jumuiya unagombaniwa hivi? kulikoni wana DMV? au kuna ruzuku zinatoka hazina? haa haa.

    ReplyDelete
  5. hii timu libe ni ya mchezo gani. maana uchaguzi tumemaliza sasa timu ya nini. mimi najua kucheza mpira wa miguu naombeni namba.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...