Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mbulu Joseph Geheri akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Mnara wa huduma za Mawasiliano katika kijiji cha Aicho wilayani Mbulu Mkoani Manyara ambapo sasa wakazi wa kijiji hicho na jijini vya jirani wameunganishwa na huduma za simu za mkononi za Airtel. Akishuhudia ni Meneja Mauzo wa Airtel Kanda ya Kaskazini Brightone Majwala pamoja na wakazi wa Kijiji hicho
Meneja Mauzo wa Airtel Kanda ya Kaskazini Brightone Majwala akiwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mbulu Joseph Geheri wakati wa uzinduzi wa Mnara wa huduma za Mawasiliano katika kijiji cha Aicho
wilayani Mbulu Mkoani Manyara. Pichani ni wakazi wa Kijiji hicho
Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel imewawezesha wakazi wa kijiji cha
Aicho na vijiji vya jirani kupata huduma za mawasiliano kufatia
uzinduzi wa mnara wa mawasiliano katika kijiji cha Aicho kata ya
Marang wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara
Uzinduzi huo ni mwendelezo wa dhamira ya Airtel katika kuboresha
upatikanaji wa mawasiliano na kuwawezesha wakazi wa maeneo ya
pembezoni mwa nchi kupata huduma ya mawasiliano ya simu za Mkononi
Akiongea wakati wa uzinduzi uliofanyika mkoani Manyara Meneja Mauzo
kanda ya kaskazini wa Airtel Bwana Brighton Majwala alisema “ Airtel
Tunatambua kuwa mawasiliano ni kichocheo kikuu cha uchumi katika
nchini na jamiii yoyote ile, ndio maaana tumeona ni vyema kufikisha
mawasiliano katika maeneo yenye changamoto za mawasiliano hususani ya
vijijini. Na leo tunazindua huduma za mawasiliano katika kijiji cha
Aiko na kuwawezesha wakazi wa hapa na maeneo ya jirani kupata huduma
mbalimbali ikiwemo za kifedha za kutuma na kupokea pesa, kufanya
malipo kwa njia rahisi, salama wakiwa mahali popote kwa kupitia
huduma ya Airtel Money”.
“Airtel tumejipanga na tutaendelea kutekeleza dhamira yetu ya kutoa
huduma bora za kibunifu na za bei nafuu na huku tukiendelea kuboresha
upatikanaji wa mawasiliano katika maeno mbalimbali ya pembezoni
nchini” aliongeza Majwala
Kwa upande wake mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya
Mbulu Joseph Geheri alisema” Tunashukuru sana Airtel kwa kuendelea
kuboresha mawasiliano na kuwapa vijana wetu kufaidika na kupata Ajira
kwa kupitia huduma hizi zilizosheheni hapa wilayani Mbulu.Kadhalika
mawasiliano haya yamewawezesha wanafunzi kupata taarifa za matokeo yao ya mtihani ya kuhitimu kwa kupitia simu za mkononi mahali popote pale walipo.
Vilevile tunafurahi kuona jinsi gani Airtel imerahisha mawasiliano
haya kijiji hapa na kuwezesha upatikanaji wa taarifa muhimu kwa wakati
na kirahisi zaidi, kwa wafanyabiashara, wakulima pamoja na wafugaji
mawasiliano haya yatawawezesha kuendesha shughuli zao za kiuchumi kwa
ufanisi zaidi na kupata masoko katika sehemu mbalimbali za nchi
kupitia mtandao huu wa simu za mkononi wa Airtel. Nachukua nafasi hii
kuwaasa wakazi wa hapa kuyatumia mawasiliano haya kwa faida ya
maendeleo yao na ya jamii kwa ujumla Aliongeza Geheri
Airtel inaendelea kupanua wigo wa mawasilano nchini ambapo wiki
zilizopita Airtel ilizindua mnara wa mawasiliano katika mkoa wa
Sigunga Kigoma na Muhukuru Songea , huku ikiwa na mpango mkakati wa
kuzindua huduma za mawasiliano katika maeneo mengi zaidi nchini. Sasa
wakazi wa sigunga, Mahukuru na Aicho wanafurahia huduma mbalimbali za
Airtel ikiwemo ya kifedha ya Airtel Money Hatoki Mtu hapa, Switch on
huduma ya internet na vifurushi vya Airtel yatosha na vingine vingi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...