
Taarifa ya DIT kwa vyombo vya habari imesema kuwa tuzo kwa wanafunzi
zitatolewa Januari 23 mwaka huu ikiwa ni wiki moja kabla ya mahafali hayo
ambayo wahitimu katika ngazi na masomo tofauti watatunukiwa.
Wahitimu watakaotunukiwa ni siku hiyo ni pamoja na wa Stashahada ya
Uhandisi (Ordinary
Diploma), cheti cha awali cha TEHAMA (IT) mwaka wa masomo 2013/2014.
Wahitimu wametakiwa kusoma
utaratibu wa kuthibitisha kushiriki mahafali hayo katika tovuti ya Taasisi www.dit.ac.tz na “Rehearsal”
itafanyika Ijumaa tarehe 30 Januari 2015.
“Malipo ya
Tshs 30,000/= kwa ajili usajili yatafanyika kwenye tawi lolote la NBC kwenye akaunti namba 018101003145 na
kujisajili kupitia tovuti ya Taasisi www.ac.dit.tz” Inasema taarifa hiyo.
Malipo yanatakiwa
klufanyika kwa kutumia jina kamili kama linavyoonekana kwenye orodha ya wahitimu
iliyotolewa kwenye tovuti ya Taasisi, namba ya usajili na dhumuni la malipo mf.
Ada, transcript na graduation.
Kulingana na
taarifa hiyo, mwisho wa kujisajili ni tarehe 31 Desemba, 2014 na wahitimu wametakiwa kufahamisha
kuhusiana na mahafali hayo.
IMETOLEWA NA UONGOZI DIT
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...