Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umenyakua tuzo tatu za ubunifu katika sekta ya hifadhi ya Jamii Barani Afrika zinazosimamiwa na Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Duniani (ISSA).

Halfa ya kukabidhi tuzo hizo ilifanyika Jijini Casablanca nchini Morocco usiku wa tarehe 3 Desemba, 2014 katika hoteli ya Serana jijini Casablanca ambapo washiriki zaidi ya 360 kutoka taasisi 75 katika mataifa 45 ya Afrika zilihudhuria.

Tuzo ambazo NHIF ilikabidhiwa ni katika eneo la utoaji wa huduma za matibabu za kibingwa maeneo magumu kufika, kazi ambayo mfuko umefanya kwa kushirikiana na wataalamu wa hospitali za rufaa nchini. tuzo nyingine ni katika eneo la TEHAMA katika utayarishaji madai na huduma za matibabu kwa wanachama wastaafu.

Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo wa Kanda ya Afrika ambacho pia kilijadili mambo muhimu kuhusu sekta ya hifahi ya jamii na kutambua kazi za ubunifu uliongozwa na Waziri wa kazi Mheshimiwa Gaudensia Kabaka pamoja na Viongozi waandamizi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii nchini (SSRA) na baadhi ya Watendaji wakuu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini.

Tangu kuanza kutolewa kwa ambazo hushindaniwa kila baada ya miaka mitatu, NHIF imeng'ara mara zote.Mwaka 2008 ilipata tuzo ya cheti cha heshima cha ubunifu mjini Kigali kwa kuwashirikisha wadau wake katika utoaji wa elimu kwa makundi mbalimbali ngazi ya mkoa. Mwaka 2011 ulikuwa mshindi wa kwanza wa jumla barani Afrika na mwaka huu umeibuka tena na ushindi huo muhimu unaoitangaza Tanzania kimataifa kupitia Bima ya Afya.

Mbali ya NHIF, Tanzania pia imengara kwa kuzoa jumla ya tuzo 6 mbapo Mamlaka ya Udhibiti ya SSRA, Mfuko wa Pensheni wa PPF na Mfuko wa PSPS pia ilijizolea tuzo moja moja kwa kila mmoja hivyo kufanya Tanzania kuwa na jumla ya tuzo 6 na kuifanya kuwa kinara katika ukanda wa nchi za Afrika mashariki na ya Kati.

Mifuko ya Hifadhi ya Jamii katika nchi nne ilipata heshima ya pekee kwa kazi zao za ubunifu. Mifuko hiyo ni kutoka Cameroon yenyewe iliyonyakua tuzo 8, Gabon, Maurtania, wenyeji Morocco.

Washindi wa jumla wa kwa mwaka 2014 ni wenyeji Morocco na Jirani zao wa Mauritania ambao kwa pamoja wamepata tuzo ya jumla kwa kutoa huduma bora, kuongeza uwigo wa wanaonufaika na huduma za mifuko hiyo hasa wasio na uwezo, matumizi ya TEHAMA na huduma kwa wateja na ufanisi kwa ujumla.
Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Hamis Mdee (wa pili kulia) akikabidhiwa Tuzo za Ubunifu ambazo NHIF ilinyakuwa tuzo 3 Barani Afrika Mjini Casablanca Mwishoni mwa Juma. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...