Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Comoro,Mhe. Chabaka Kilumanga ameshiriki katika shughuli ya kuwakumbuka wahanga wa mashambulizi ya kigaidi yaliyofanywa katika Ofisi za Charlie Hebdo, jijini Paris, Ufaransa. Shughuli hiyo, iliyoandaliwa na Balozi wa Ufaransa nchini Comoro na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Comoro, Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa pamoja na watu mashuhuri, iliambatana na kusaini kitabu cha maombolezi.
Mhe. Balozi Chabaka Kilumanga akisalimiana na Mhe. Ahmed Abdallah Mohamed Sambi, wakati akiwasili katika maombolezi ya mashambulizi ya Charlie Hebdo.
Mhe. Balozi Chabaka Kilumanga akisaini Kitabu cha Maombolezi ya Wahanga wa Mashambulizi ya Charlie Hebdo. Kushoto, aliyesimama ni Balozi wa Ufaransa nchini Comoro.
Angalao pia watie saini kitabu cha maombolezo kwa wahanga wa Nigeria ambao melfu wameisha uwawa.
ReplyDelete