Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakurugenzi wa Chama cha Ushirika cha Ujenzi wa Nyumba Mwenge
(MHCS Ltd), Hillaly Mdaki akizungumza wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo, uliofanyika Afrika Sana
Mwenge jijini Dar es Salaam.Kulia ni makamu mwenyekiti wa bodi hiyo, Hellena Khamsini.
Mjumbe mmojawapo wa bodi ya hiyo, Ndesumbuka Merinyo akisaini hati ya kiapo cha kuitumikia nafasi hiyo katika hafla iliyofanyika Sinza, Afrika Sana jana.
Bodi Mpya ya Wakurugenzi wa Chama cha Ushirika cha Ujenzi wa Nyumba Mwenge (MHCS
Ltd), imezinduliwa rasmi jana ambayo pamoja na mambo mengine, imejizatiti kuhakikisha
inatekeleza miradi ya maendeleo kwa ajili ya wanachama wake.
Akizungumza mara baada ya kuapishwa, mwenyekiti wa bodi hiyo Hillaly Mdaki alisema kuwa
pamoja na mambo mengine itahakikisha inatekeleza miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na ile ya
ujenzi wa majengo pacha yenye urefu wa ghorofa 32 katika kiwanja ilipo Afrika Sana, Sinza jijini
Dar es Salaam.
Pia ujenzi wa nyumba za wanachama na vitegauchumi vingine kupitia mikopo ya mabenki katika
eneo la kiwanja chenye ukubwa wa ekari 800 katika eneo la Kibiki, Chalinze mkoa wa Pwani.
Mdaki alisema serikali kupitia mrajisi wa vyama vya ushirika imewakabidhi eneo hilo Chalinze na
wanachama 378 tayari wamekabidhiwa viwanja na hati za umiliki wa viwanja hivyo na awali
waliomba Bagamoyo lakini wakapatiwa Chalinze, jambo ambalo alisema ni jema.
“Lengo ni kuhakikisha wanachama ambao wengi wao ni wastaafu wa serikali wananufaika na
ushirika” alisema na kuongeza kuwa bodi iliyozinduliwa pamoja na mambo mengine ina jukumu la
kuhakikisha ujenzi wa nyumba hizo za wanchama unakamilika na kupitia mikopo ya mabenki.
“Pia bodi ina jukumu la kuhakikisha mradi wa majengo pacha yatakayokuwa na jumla ya ghorofa
32 ikiwa ni idadi ya 16 kila upande unakamilika” alisema na kuongeza kuwa michoro kwa ajili ya
ujenzi huo imekamilika.
Alibainisha kuwa majengo hayo pacha yatajengwa katika kiwanja hicho ilipo Afrika Sana, eneo
ambalo walipewa na Rais wa Awamu ya Kwanza, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere mwaka 1971 na pia wamelenga kutekeleza miradi kadhaa ya ujenzi mikoani pia.
Tupo Mwenge ambayo ni alama ya mwangaza kwa nchi nzima hivyo nasi tutatekeleza miradi hiyo
ya ujenzi katika mikoa mingine 10 nchini kwa kuanzia lengo kufanya hivyo nchi nzima” alisema na
kuongeza kuwa viwanja 77 vitagawiwa kwa wakazi wengine wa jiji ambao watahitaji.
Awali mwenyekiti anayemaliza muda wake, aliwataka wajumbe na mwenyekiti mpya kufanyakazi
kwa kufuata kanuni, sheria ya vyama vya ushirika na katiba na alibainisha kuwa hadi kufikia ulipo
huo ushirika ni jitihada binafsi za wanachama.
Sasa nimeelewa historia ya Afrika Sana, Sinza Mwenge jijini Dar-es-Salaam na influence ya Baba wa Taifa juu ya dhana ya Ujamaa na Kujitegemea kama hawa Wanachama wanavyojipanga kujitegemea kwa vitendo.
ReplyDeleteHongereni sana.