Home
Unlabelled
TAARIFA KWA UMMA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Sasa na hayo makampuni ya nje yanayochimba madini na kupeleka na ndege zao moja kwa moja kutoka machimboni mtajuaje?Naona hii ni kutaka kuwabana wafanya biashara wadogo wadogo huku mnafumba macho mabedui.Angalia dhahabu inavyoibwa lakini msemi chochote kweny hayo makampuni ya nje.
ReplyDeleteHiyo tarehe mbona haijafika!!!!!
ReplyDeleteMakampuni ya nje yanayochimba dhahabu na kupeleka na ndege moja kwa moja kutoka machimboni hiyo procedure inafanywa mtu wa TMAA akiwepo kuangalia dhahabu kiasi gani mesafirishwa na huwezi pewa kibali cha kusafirisha kama hujalipa royalties. Watanzania wengi hawaelewi wanaishi kulalamika tu
ReplyDeleteHata Makampuni ya nje yanaaangalia . Manake katika kila mgodi wapo Maafisa Wa Wakala Wa Ukaguzi wa Madini Tanzania(TMAA) ambao wanakuwepo katika kila hatua toka za awali hadi mwisho. Lakinipia kuna kamati nzima ya ulinzi , kuna polisi Usalama wa Taifa kwa hiyo hakuna. Kwa hiyo zoezi hili halilengi wachimbaji wadogo au wafanyabiashara wadogo ni wote. We toa taarifa tu zitafanyiwa kazi.
ReplyDeleteMakampuni ya nje pia yanaangaliwa kwasababu katika kila mgodi wapo wataalamu kutoka Wakala wa Ukaguzi Tanzania (TMAA) kuhakikisha wanafanya ukaguzi na kufuatilia taratibu zote. Mbali na hao kuna polisi kuna watu wa usalama. Kwa hiyo taarifa hii haiwalengi wafanyabiashara wadogo au wachimbaji wadogo tu ni wote. Ukitoa taarifa zitafanyiwa kazi.
ReplyDeleteUfafanuzi kwa Mdau Hapo Juu: Kutokana na thamani ya madini na kwa kuzingatia usalama wa madini na wasafirishaji ni hatari kusafirisha madini kutoka mgodi wowote kwenda Mwanza au Dar es Salaam kwa gari, hivyo migodi inalazimika kusafirisha kwa ndege au helikopta. Pia, kwa mujibu wa sheria na taratibu za usafiri wa anga ni lazima ndege ipewe ruhusa na njia ya kupita kabla ya kuruka, vilevile hairuhusiwi ndege kusafiri kutoka kwenye kiwanja cha mgodi kwenda nje ya nchi. Ndege zote zinasafiri kwa vibali maalum na hivyo ndege haziwezi kutumika kwa ajili ya utoroshaji wa madini.
ReplyDeletePamoja na maelezo hayo, kabla madini hayajasafirishwa kutoka mgodini lazima taratibu za kuhakiki na kuthibitisha madini zifanyike. Hivyo, wakaguzi wa Wakala wa Ukaguzi Madini (TMAA), TRA, maofisa wa madini wa kanda husika na maofisa usalama wanahusika kuhakiki madini husika kabla ya kuruhusu kusafirishwa kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar es Salaam, Mwanza na Kilimanjaro.
Kwa tangazo hili Serikali inaomba wananchi wote kutoa ushirikiano ili kudhibiti utoroshaji madini kwa maslahi ya Taifa.
yaani mtoa taarifa akae anasubiri muyauze hayo madini tu..je ikichukua miezi sita? kumbukeni thamani ya pesa inashuka kila kukicha. milioni moja ya leo si milioni moja ya miezi sita ijayo. kwakufanya hivyo mtasababisha isiwe siri tena maana mtoa taarifa anaweza akaanza kuilalamikia mamlaka husika kwa ucheleweshaji huo na hatimae taarifa zikavuja. Mi nashauri, hivi kwanini msitenge fedha kwa ajili ya malipo husika kwa watoa taarifa, then mkiuza mnarudisha mlikotoa? lakini pia natoa angalizo, msije tumia malipo hayo kama kichaka cha ufisadi kwa maana ya kinachotoka kama malipo kwa mtoa huduma kifanane na atakachopokea..... kisije kikatoka kikubwa na kikapokele kidogo.
ReplyDeleteMungu Ibariki Tanzania