Shika ndinga kwa wilaya ya Kinondoni imefanyika leo Aprili 4,2015 katika uwanja wa Garden Kinondoni jijini Dar es salam,ambapo wasikilizaji wa Radio EFM waliopata nafasi ya kushiriki baada ya kujibu maswali mbalimbali kupitia vipindi vya redio walishindana kushika ndinga ili kuweza kujishindia ndinga ya biashara.
Washiriki wa shindano kwa Wanawake walikua 21 na wanaume 20 ambapo kati ya hao ni Wanawake Watano na Wanaume watano waliofanikiwa kuendelea mbele katika raundi nyingine ambapo watashiriki katika fainali na washindi wengine kutoka katika Wilaya ya Ilala na Temeke.
Mtiririko wa kushika ndinga ulikuwa ni kusimama kwa miguu miwili wakiwa wameshika ndinga na baada ya kama dakika tano wanaume wengi walianza kushuka baada ya kushindwa kuhimili vigezo vilivyowekwa na wanawake walisimama imara kwa muda na badae wao walianza kushindwa kwa wingi kuliko wanaume.
Ndani ya lisaa la kwanza tu washindi watano wanawake walipatikana hivyo zoezi hilo kubaki wanaume tu, ambao baada ya muda kidogo walibadilishiwa zoezi la kushika ndinga kwa mguu mmoja na mwingine kuuinua usishuke chini chini hapo ndipo washindi Watano Wanaume walivyopatikana.
Washindi kwa upande wa Wanawake ni KHADIJA RASHIDI, SWAUMU IDDI, HAPPY AMBROS, NYABUHO Peter na HABIBA,
Na kwa upande wa Wanaume ni ABDUL Said , KASSIM Said, ERNEST EDWARD, MUBARAK RAMADHANI pamoja na MBWANA KASANGA.
Very creative radio station na wameweza kuteka masikio ya watu
ReplyDelete