Awamu ya tatu ya Kundi la Watanzania waliokuwa wakiishi nchini Yemen, wameendelea kurudishwa nyumbani kutokana na mapigano yanayoendele nchini humo. Watanzania 40 ambao walikimbilia nchini Oman kutokea Yemen, wamefanikiwa kusafirishwa leo chini ya usimamizi wa Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mh. Ali Ahmed Saleh.
Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mh. Ali Ahmed Saleh akizungumza na Baadhi ya watanzania waliokuwa wakiishi nchini Yemen, ambao wako safarini hivi sasa kurudishwa nyumbani baada ya mapigano yanaoendelea nchini humo.

Awamu ya Tatu yenye jumla ya Watanzania 39 kutoka Yemen wanatarajiwa kuwasili nchini tarehe 06 Mei, 2015 ikiwa ni jitihada za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwarejesha nyumbani kufuatia mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yanayoendelea nchini humo.

Watanzania hao wakiwemo Wanafunzi watawasili nchini kwa Ndege ya Shirika la Qatar namba QR 1349 majira ya saa 1.55 (saa moja) asubuhi.

Kurejea kwa Watanzania hao kutafanya jumla ya Watanzania waliorejea kutoka Yemen hadi hivi sasa kuwa 62 kati ya   Watanzania 69 waliojiandikisha kurudi  huku jitihada za kuwaandikisha wengine zikiendelea kufanywa na Ubalozi wa Tanzania nchini Oman.

Awamu ya kwanza ya Watanzania waliorejea ilihusisha familia ya watu watano huku awamu ya pili ilikuwa na Watanzania 18.

Itakumbukwa kuwa, hivi karibuni Serikali kupitia Waziri wa Mambo  ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe ilitangaza kuwarejesha nchini Watanzania waliopo Yemen kufuatia machafuko yanayoendelea nchini humo.


IMETOLEWA NA: WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM.
05 MEI, 2015

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...