Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
WAKALA wa usajili ufilisi na udhamini(RITA) wamewataka wazazi na walezi wanaosoma shule za msingi za Manispaa ya Kinondoni wawaandikishe watoto wao ili waweze kupata vyeti vyao vya kuzaliwa.

Hayo yamesemwa na Meneja masoko Mawasiliano na Elimu kwa Umma wa RITA Josephat Kimaro  wakati akizungumza na wandishi wa habari katika ukumbi wa Habari MAELEZO leo jijini Dar es Salaam.

Kimaro amesema kuwa wananchi wajue umhimu wa cheti cha kuzaliwa kwani Cheti cha kuzaliwa ni nyaraka inayodhibitisha taarifa muhimu za wananchi ikiwa ni pamoja na  tarehe ya kuzaliwa, mahali alipozaliwa, wazazi halisi na miliki halali wa cheti.

Pia Kimaro amesema kuwa  kila shule ya msingi ya Manispaa ya Kinondoni wameteua Mwalimu mmoja  ili kuhakikisha kila Mwanafunzi anapewa cheti cha kuzaliwa.

Amesema kuwa zoezi la uandikishaji  wa wanafunzi wa shule za msingi katika Manispaa ya Kinondoni, walioomba na waliopewa vyeti katika shule hizo ni wanafunzi 5081 kati ya hao ni wasichana 2720 na wavulana 2361.
 Meneja masoko Mawasiliano na Elimu kwa Umma wa RITA Josephat Kimaro akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani katika ukumbi wa habari MAELEZO jijini Dar es Salaam leo, kulia ni Msajili wa vizazi na vifo Mariam Ling'ande.
 Msajili wa vizazi na vifo Mariam Ling'ande akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,kushoto ni Meneja masoko Mawasiliano na Elimu kwa Umma wa RITA Josephat Kimaro.
 Baadhi ya wandishi wa habari waliohudhulia katika mkutano na 
Wakala wa usajili ufilisi na udhamini(RITA) jijini Dar es Salaam leo.(PICHA NA EMMENUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...