Kaimu Mkurugenzi Idara ya Diaspora kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa Bi. Rosemary Jairo akiongea na waandishi wa Habari
kuhusu Maandalizi ya Kongamano la Diaspora (Tanzania and SMEs Partnership
Conference 2015) litakalofanyika kuanzia tarehe 13-15 Agosti 2015 Jijini Dar es
Salaam.Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO), Leo Jijini
Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Idara ya
Diaspora kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bi.
Rosemary Jairo.
Picha na Hassan Silayo-MAELEZO
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na
Kituo cha Uwekezaji cha Kimataifa (International Trade Centre
UN-Agency) inafanya Maandalizi ya Kongamano la Diaspora
(Tanzania Diaspora & SMEs Partnership Conference 2015).
Kongamano husika litafanyika hapa Dar es Salaam, kuanzia tarehe
13 hadi 15 Agosti 2015 katika Hoteli ya Serena. Kongamano hilo
litakuwa la pili kufanyika hapa nchini na litahusisha Diaspora na
Wadau wa hapa Tanzania.
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ofisi ya Rais
na Utawala Bora – Zanzibar na Ofisi ya Waziri Mkuu ndio Wadau
Wakuu katika Maandalizi ya Kongamano hili.
Kongamano la mwaka huu lina Kauli Mbiu, ‘Creating Linkages
between Diaspora and Local SMEs in Tanzania’ na Dhumuni
lake ni kuhamasisha Ushiriki wa Diaspora katika kukuza Biashara
Ndogo na za Kati hapa nchini. Kongamano la mwaka huu pia
litahusisha Mikoa ya Tanzania ambapo Mikoa itapata fursa ya
kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo Mikoani.
Kongamano hilo linatarajiwa kufunguliwa na Mhe. Jakaya Mrisho
Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kufungwa
na Mhe. Dr. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi.
Aidha, katika kuhitimisha kilele cha Kongamano hilo, Diaspora
wanatarajiwa kufanya ziara Zanzibar tarehe 15 Agosti 2015, ikiwa
ni sehemu ya mwaliko maalum kutoka Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar.
Pamoja na Shughuli za Ufunguzi na Kilele, Matukio muhimu
yatakuwa ni Maonesho ya Kibiashara, Majadiliano ya Mada kuhusu
Ushirikishwaji wa Diaspora kwa Maendeleo ya Nchi hususan SMEs,
uwekezaji Mikoani n.k.
Kongamano hilo litahudhuriwa na Watanzania Wanaoishi
Ughaibuni (Diaspora) na wale waliorejea hapa nchini na Wadau
wa Maendeleo kutoka hapa nchini.
Wizara ya Mambo ya Nje inawakaribisha kushiriki nasi katika
Kongamano hilo. Tafadhali tembeleeni tovuti ya
(www.tzdiaspora.com) kupata taarifa muhimu hususan kuhusu
Ada za Ushiriki, fursa za Kufadhili na namna ya kujisajili.
Imetolewa na: Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Dar es Salaam
21 Julai, 2015
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...