Waziri wa Kazi Viwanda na Ustawi wa Jamii wa Sierra Leone Dk. Methew Teambo na wawakilishi wa mamlaka za afya kutoka nchini Sierra Leone wakiambatana na maasifa wa mfuko wa bima ya afya Tanzania (NHIF) wemefanya ziara ya mafunzo katika hospitali ya Kairuki iliyopo Mikocheni jijini, Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo ya mafunzo wameweza kuona utaratibu wa Kairuki Hospital wa jinsi wanavyowahudumia wateja wa NHIF ambapo waziri na wawakilishi kutoka Sierra Leone walikuwa na lengo la kuja kujifunza.

Pamoja na kupata mafunzo hayo, pia waziri na wawakilishi wake wameweza kutembelea sehemu mbali mbali na kujione vifaa vya kisasa vilivyopo katika hospitali hiyo. Akizungumza baada ya ziara hiyo, waziri amesema “utaratibu huu wa NHIF ni mzuri kwani unashirikiana na sekta binafsi katika kuwapatia huduma za afya wanachama na wananchi kwa ujumla”.

Hata hivyo, waziri amemshukuru Mkurugenzi wa hospital hiyo Dr Asser Mchomvu  kwa kukubali  kuwapatia mafunzo  hayo na  kuapatia maelezo ya  kina ya jinsi NHIF ilivyosaidia  kutoa mwanga kwa namna mbali mbali kwa vituo vya afya kuweza  kufanyakazi na mfuko huo katika kutoa huduma kwa wanachama wa mfuko huo.

 Waziri wa Kazi Viwanda na Ustawi wa Jamii wa Sierra Leone Dk. Methew Teambo akiwa Ndani ya chumba cha CT SCAN machine ya kisasa inayotumika kuchunguza maradhi mbalimbali ya binadamu alipotembelea Hospitali ya Kairuki.
Waziri akipiga picha kwenye chumba cha mammography Mashine ya kuchunguza saratani ya matiti (Mammography).

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...