KWAYA ya Uinjilisti ya
Kijitonyama imechomoza kumsindikiza mwimbaji nguli wa muziki wa Injili
Tanzania Bonny Mwaitege anayetarajia kuzindua albamu tatu, uzinduzi
unaotarajia kufanyika Agosti 2 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini
Dar es Salaam.
Sambamba na Kwaya hiyo pia uzinduzi
huo utasindikizwa na mwimbaji mwingine mahiri Afrika Mashriki na Kati,
Joshua Mlelwa ambaye ni machachari zaidi awapo jukwaani.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama uzinduzi huo
unatarajia kusindikizwa na waimbaji mbalimbali wa Tanzania na nje lengo
likiwa ni kufanikisha uzinduzi mahiri wa albamu hizo.
Msama
alisema pamoja na uzinduzi huo kusindikizwa na waimbaji mahiri pia,
waimbaji chipukizi watamsindikiza Mwaitege ambaye hivi sasa anaendelea
na mazoezi kuelekea uzinduzi huo.
Aidha Msama
alisema hivi sasa muimbaji huyo pia anamalizia kurekodi baadhi ya nyimbo
zilizomo kwenye albamu hizo katika majiji ya Mwanza, Arusha, Mbeya na
Nairobi.Msama alisema uzinduzi huo baada ya
kufanyika Dar es Salaam, Agosti nane utahamia Wilayani Makambako mkoani
Njombe na siku inayofuata watazindua albamu hizo kwenye uwanja wa
Sokoine jijini Mbeya.
msama
alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa mashabiki wa muziki wa injili
kujiandaa na uzinduzi huo ambao utakuwa ni wa aina yake."Maandalizi
makubwa kuelekea uzindizu wa Mwaitege yameshafanyika, kilicho mbele ni
uzinduzi wa hali ya juu, mashabiki wakae mkao wa kula," alisema Msama na
kuongeza.
"Uzinduzi wa Mwaitege utakuwa ni wa aina
yake kwa sababu maandalizi yake kwa sababu yamefanywa kwa ustadi mkubwa,
mashabiki watarajie kazi bora zaidi kutoka kwa muimbaji huyo," alisema.
Bonny Mwaitege anatamba na nyimbo mbalimbali kama
Mama ni Mama, Mke mwema, Wakusamehe, Fungua Moyo wako, Njoo uombewe na
Yesu yupo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...