
Naibu waziri wa maendeleo ya jamii jinsia na watoto Dkt
Shirika la mawasiliano la TTCL Tanzania limekabidhi jumla ya bati 100
zenye thamani ya shilingi Milioni mbili kwa Mbunge wa viti maalumu
mkoa wa Njombe Dokta Pindi Hazara Chana ambaye pia ni Naibu waziri wa
maendeleo ya Jamii Wanawake jinsia na watoto kwa ajili ya sekta
ya elimu mkoani Njombe.
Akikabidhi bati hizo kwa niaba ya mkurugenzi kuu wa TTCL
Tanzania, Kaimu mkurugenzi kanda ya nyanda za Juu kusini bwana James
Mlaguzi amesema kwa kuwa shirika hilo limekuwa likifanya kazi za
kijamii kupitia mapato yake hivyo limeamua kuchangia sekta ya Elimu
mkoa wa Njombe kupitia Mbunge Chana kwa kutoa bati hizo.
Amesema katika mkoa wa
Njombe wametoa jumla ya bati 100 ambazo zitasaidia kupunguza
changamoto katika ujenzi wa madarasa na maabara katika shule
mbalimbali.
Aidha mara baada ya
kukabidhiwa bati hizo, Naibu waziri Chana na msafara wake pamoja na
TTCL wameelekea katika shule ya Sekondari Mbeyela ambako amekabidhi
bati 20 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa.
Taarifa fupi ya
shule ya Mbeyela Sekondari iliyosomwa na mkuu wa shule hiyo Mwalimu
Emphraim Ngimba imeeleza kuwa shule hiyo yenye zaidi ya wanafunzi 500
na walimu zaidi ya 50 zitasaidia kupunguza adha ya ukarabati wa
madarasa kutokana na madarasa mengi kutokamilika.

Akizungumza na wanafunzi
wa shule hiyo wakati wa kukabidhi bati hizo 20 Mbunge Pindi Chana
ametumia fursa hiyo kuwataka wanafunzi hao kujikita zaidi katika
masomo ili waje kuwa viongozi makini katika Taifa la
Tanzania.
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...