Spika wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda amesema wanawake bado wanateseka takribani kote duniani, wengine wakiambulia vipigo na kadhia mbalimbali.
Kandoni mwa mkutano wa Nne wa maspika wa mabunge duniani jijini New York spika Makinda amemueleza Joseph Msami wa idhaa hii, spika huyo wa kwanza mwanamke nchini Tanzania anasema lazima wanaume na jamii kwa ujumla wamkomboe mwanamke. Kwanza anaanza kueleza maudhui ya mkutano.
KUSIKILIZA BOFYA HAPA
Wanawake wakiwezeshwa kielimu na kiuchumi wataweza kujisimamia, na kujithamini wawe wameolewav au hawajaolewa wanaweza kutoa mchango mzuri katika familia zao walizozaliwa, za kuolewa na katika taifa kwa ujumla. Wanawake wanahitaji kujitambua na kutafuta kujiendeleza na kujitegemea zaidi kuliko walivyo sasa hapa nchini.
ReplyDelete