TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Agizo alilolitoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la kutaka fedha zilizochangwa na wadau mbalimbali kwa ajili ya kugharamia hafla ya wabunge zipelekwe Katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kununulia vitanda na magodoro ya wagonjwa wanaolala chini limetekelezwa.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema fedha hizo zimefanikisha kupatikana vitanda 300 vya wagonjwa pamoja na magodoro yake, shuka 600, Baiskeli za kubebea wagonjwa na vifaa vingine na kwamba hivyo vyote tayari vimepelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Balozi Sefue ameuagiza uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha vitanda vyote vinafungwa kesho jumapili na kwamba atakwenda kuvikagua siku ya jumatatu vikiwa tayari vinatumiwa na wagonjwa waliokua wanakosa vitanda vya kulalia na kulazimika kulala chini.

Wadau mbalimbali walichanga fedha kiasi cha shilingi milioni 225 kwa ajili ya kugharamia hafla ya wabunge baada ya uzinduzi rasmi wa bunge la 11 lakini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli aliagiza fedha hizo zitumiwe kwa kiasi kidogo kisichozidi shilingi milioni 15 na nyingine zipelekwe hospitali ya Muhimbili kutatua tatizo la uhaba wa vitanda.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano IKULU,

Novemba 21, 2015.
 Magari ya Bohari ya Dawa (MSD), yakishusha vifaa tiba Taasisi ya Moi kufuatia agizo la Rais Dk.John Magufuli kulitaka Bunge kutumia sh.milioni 15 kwa ajili ya kujipongeza na fedha zilizobaki kuzipeleka katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kukabiliana na uhaba wa vifaa tiba na magodoro. 
BOHARI ya Dawa (MSD) imeanza kupeleka Vifaa Tiba kwenye Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI), Vifaa ambavyo vimenunuliwa na Ofisi ya Bunge kwa agizo alilotoa Rais Dk. John Magufuli. Vifaa hivyo vilianza kupelekwa juzi katika Taasisi hiyo ili kukabiliana na uhaba alioubaini Rais  Magufuli baada ya kufanya ziara ya kushitukiza katika mapema mwezi huu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Balozi Sefue na Rais mbarikiwe sana. Tunawafagilia. Mungu awalinde.

    ReplyDelete
  2. Maslahi ya taifa; sio ya ubinafsi.

    Hata hafla nyingine za wizara na mashirika ya umma (wakati mwingine kufanya mashindano ya kufukuza kuku - ukatili wa wanyama na ndege)nazo zisitishwe na pesa hizo siboreshe hospitali zetu, kwanza.

    ReplyDelete
  3. Tanzania Tanzania
    Nakupenda kwa moyo wote
    Nchi yangu Tanzania
    Jina lako ni tamu sana
    Nilalapo nakuota wewe
    Niamkapo ni heri mama wee
    Tanzania Tanzania
    Nakupenda kwa moyo wote
    HAPA KAZI TU.

    ReplyDelete
  4. Tulichohitaji ni rais mwenye roho ya huruma kwa wananchi wake and it seems like JPM is right person for that. Yaani kali ya mtu 1 tu, vitanda 300 na some change chaaa. Hii kitu iendelee kwa viongozi wa mikoa na wilaya kwenye hospitali zao. Pesa nyingi zinatumika kwenye vikao na sherehe zisizo na tija, mkifuata mfano wa bosi wenu matatizo ya afya na elimu yatakuwa historia. Mungu mbariki raisi wetu JPM, Mungu ibariki Tanzania yetu

    ReplyDelete
  5. Sasa hospitali kubwa kama muhimbili kila mkoa.

    ReplyDelete
  6. Tuzidi kumuomba Mungu ili Watanzania wote tuwe na Moyo kama huu.Asanre sana Rais wetu kwa kuwa mfano bora.
    Wananchi wote tuhamasishane ili sote tuwe katika muelekeo huu ili tuzidi kuijenga Nchi yetu

    ReplyDelete
  7. kama unataka ukusanyaji wa kodi kubwa basi tumia tecknologia (electronic). Kila mwenye duka awe na mashine ya electronic na matandao iripoti TRA mauzo yote kimtandao.

    majuu wanafanikiwa hivyo.

    makaratasi ndo hayo yanaleta mizengwe.

    Muuza duka anuliza unataka risiti? kama unataka ungeza 20% ya vat. Teknologia itaondoa swali hilo. Ila inahitaji mtaji na elimu.

    ReplyDelete
  8. Sisubiri. Naanza kupendekeza katiba iruhusu kuwa raisi kwa zaidi ya miaka 10 ili huyu jamaa atumikie watu kwa muda mrefu.

    Halafu akiondoka tutabadili iwe miaka 5 siyo 10 tena. Maana kunyimwa maendeleo kwa miaka 10 na raisi mzembe ni hasara kubwa saana.

    ReplyDelete
  9. Thank you President John Magufuli. Thank you Chief Secretary Ombeni Sefue. If you work closely like what we see for sure our country will prosper. May Almight God give you strength and bless you aboundantly.

    ReplyDelete
  10. Namna hii unafikiri kuna haja ya kuwaangaisha wananchi na michango isiyo na mwaisho? Mara mahabara, mara rimu, mara choo, mara dawati....

    Matumizi yakipunguzwa vizuri, na kdoi yote ikakusanywa, tuatjitosheleza kila sekta. Na ndo hapa akina Mnyika waliposema kuwa serikali iliyopita ilikuwa dhaifu, watu wakaja juu!!

    ReplyDelete
  11. Yule wa kula na kusafiri anaanza kuisoma #. Yaani Tanzania na watanzania tumeteseka sana. Miaka kumi sii mchezo.

    ReplyDelete
  12. Kweli hakuna kisichowezekana... sasa tujiulize, je kila waziri, mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya wakifanya hivi tutaacha kuendelea kweli?
    Viongozi wote inabidi waige mfano huu na si kukaa pembeni na kumuangalia rais tu!

    ReplyDelete
  13. The man puts challenges and solving problems ahead of politics and bureaucracy. We don't need demigods in our poverty stricken country. Cheers fellow Magufuri!!

    ReplyDelete
  14. Tena naona hivyo vifaa ni vichache kulingana na fedha zilizochangwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...