Na Emanuel Madafa, Mbeya
Wachezaji 22 wa mpira wa kikapu Mkoa wa Mbeya, tayari wamefanikiwa kuondoka mkoani humo kwa ajili ya  kushiriki mashindano ya Taifa CUP, yatakayofanyika  Mkoani Dodoma  November 22 hadi November 30 mwaka huu.
Wachezaji hao walishindwa kusafiri mapema kuelekea mkoani Dodoma
 kushiriki mashindano hayo  kutokana na kukabiliwa na uhaba wa fedha hali iliyofanya kuwepo na maandalizi hafifu.
Aidha kufanikiwa kwa timu hiyo kunatokana na kujitokeza kwa  Kampuni ya vinywaji baridi ya Coca Cola, Mkoa wa Mbeya pamoja na Kampuni ya Tbl , amboa wamechangia kiasi kidogo cha fedha kilicho fanikisha safari hiyo.

Akizungumzia juu ya kupokea kwa ufadhiri huo Katibu wa chama  cha mpira wa kikapu mkoani Mbeya ambaye pia ni mwalimu wa timu hiyo  , Yusuf Nyirenda, amesema kuwa wanawashukuru wadau hao kwa kujitokeza   kwa kuchangia kiasi hicho cha fedha.
Amesema kampuni ya  Coca Cola pekee imechangia kiasi cha shilingi Mil 1.5 ambapo kwa upande wa TBL  wamechangia kiasi cha shilini laki tano   hivyo watajitahidi kutumia kaisi hicho kilicho patikana  ili kushiriki mashindano hayo.
Amesema, tayari timu imekwisha ondoka   Mbeya November 21, ikiwa na wachezaji 22 kati yao wanawake 11 na wanaume 11 lakini mpaka sasa  wamefanikiwa kupata shilingi milioni 2  kati ya milioni 4,700,000 zinazohitajika.
“Kiasi cha shiringi milioni 4,700,000 zinahitajika kwa ajiri ya usafiri wa kwenda na kurudi, chakula, malazi na ada ya kushiriki mashindano haya,”alisema.
Amesema kwa dhati kabisa anaipongeza kampuni ya Coca cola kwani ndio kampuni pekee ambayo imekuwa ikijitoa mara kwa mara kusaidia timu hiyo .
Amesema kutokana na mazingira hayo baadhi ya wachezaji watalazimika kujigharamia wenyewe katika eneo la usafiri   hivyo, amewaomba wadau  na mashabiki wa mpira huo, kuendelea kjitokeza kwa wingi katika kuichangia timu hiyo ili iweze kushiriki mashindano hayo.

( Imeandaliwa na Mtandao wa 
www.jamiimoja.blogspot.com Mbeya 0759406070)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...