Vijana nchini wametakiwa kuzitumia fursa zilizopo kupitia mpango wa airtel
fursa ulioanzishwa na kampuni ya simu za mikononi ya Airtel wenye lengo la
kuwawezesha wajasiriamali kujikwamua kiuchumi na hatimaye kufikia malengo
yao kimaendeleo.
Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki katika semina ya wajasiliamali
wadogowadogo iliyoandaliwa na Airtel mkoani Dodoma kupitia mradi wake wa
Airtel Fursa ambapo mwezeshaji wa semina hiyo alikuwa Dokta Robert
Mashenene ambae ni mtaalam wa maswala ya ujasiliamaili na masoko na pia ni
muadhiri wa chuo cha biashara cha CBE Dodoma
"Vijana wa Tanzania wanapaswa kujituma zaidi kutumia fursa kama
zinazowazunguka na kuibuka na mbinu tofauti tofauti kwa lengo la kupata
ajira ndani yake na kuendeleza pato la nchi yetu badala ya kulalamikia
swala la ukosefu wa ajira mara kwa mara” alisema Mashinene
Akifundisha somo la ufafanuzi wa jinsi yakusimamia wazo na amewataka
watanzania kuachana na fikra potofu za kudhani kwamba watu wanaofanikiwa
kupitia kampuni hiyo wanakuwa wameandaliwa na badala yake wachukue hatua ya
kushiriki kwa kutuma maombi yao kama inavyoelekezwa.
Kwa upande wake Mwalimu Chacha Magasi ambaye pia ni mhadhiri kutoka Chuo
Cha Biashara cha CBE mkoani Dodoma akisaidiana na muwezeshaji huyo
anawataka vijana wasomi na wa elimu ya chini kujiajiri kwa kubuni biashara
mbalimbali na kuchngamkia fursa ya Airtel ili kupunguza tatizo idadi ya
wahanga wa ukosefu wa ajira hapa nchini kwa kuwa Airtel imeamua kuwawezesha
na kuwapatia vitendea kazi kupitia fursa
“Pigeni hodi Airtel ombeni msaada wa fursa ili kukamilisha dhamira ya
kusimamia mawazo yenu na kupunguza wimbi la vijana waliokosa ajira”
alieleza Mwali Chacha
Baadhi ya wajasiriamali 220 waliohudhuria mafunzo hayo walisema Semina hiyo
imesaidia sana kufungua fikra zao hasa juu ya namna mafunzo hayo
yalivyolenga kupanua uwezo wao mwingine wa kujiajiri na sio kusubiria tu
Nichoraus Sanga alisema mimi nimejifunza kutosubiria tena ajira kuanzia
kesho nakomaa na wazo langu la kujiajiri kupitia kilimo cha zabibu na
ufugaji wa samaki hapa Dodoma ni bidhaa zinazohitajika sana.
Mradi wa Airtel fursa ni kwaajili ya vijana nchini, Ili kijana aweze
kufaidika au kushiriki kwenye Airtel Fursa atatakiwa kutuma ujumbe mfupi
kwenda kwa namba 15626 na kuweka maelezo yafuatayo:- Jina, Umri, aina ya
biashara na eneo.
Pia wanaweza kutuma maombi yao kwa kupitia barua pepe
airtelfursa@tz.airtel.com ambapo watatakiwa kutuma jina kamili, umri, na
aina ya biashara.
Maelezo kuhusu program ya Airtel FURSA pia yanapatikana kwenye tovuti ya
Airtel *www.airteltanzania.com
Meneja uhusiano wa Airtel Jackosn Mmbando akielezea kwa wajasiliamali wadogo wadogo jinsi vijana wanavyoweza kufanya ili kufaidika na mradi wa Airtel Fursa muda mfupi kabla ya kuanja kwa mafunzo yao ya
ujasiliamali yaliyodhaminiwa na Airtel Fursa maalum kwa vijana wa Dodoma mwishoni mwa wiki hiii.
Mwalimu wa ujasiliamha katika semina ya Airtel FURSA Dokta Robert Mashenene ambae pia ni muadhiri wa chuo cha biashara cha CBE Dodoma akifafanua jambo kwa vijana waliohudhuria semina ya Airtel Fursa mkoani
Dodoma kuhusu jinsi kijana anavoweza kukamata fursa na kuzitumia fursa zinazonazomzunguka kuleta maendeleo kwa jamii.*
Mmoja wa vijana Godlove Mato akipokea cheti cha ushiriki wa mafunzo
ya ujasiliamali toka kwa meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando, mafunzo
hayo yaliandaliwa na mradi wa kuwawesha vijana wa Airtel Fursa mkoni Dodoma
mwishoni mwa wiki
Mmoja wa vijana Godfrey Lymo akipokea cheti cha ushiriki wa mafunzo ya ujasiliamali toka kwa Dokta Robert Mashenene ambae pia ni muadhiri wa chuo cha biashara cha CBE wakati wa mara baada ya kumaliza kuongoza mafunzo hayo yaliyoandaliwa na mradi wa kuwawesha vijana wa Airtel Fursa mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki
Mwalimu Chacha Magasi ambaye pia ni mhadhiri kutoka Chuo Cha Biashara cha CBE mkoani Dodoma akiwashauri vijana wasomi na wa elimu ya chini kujiajiri kwa kubuni biashara mbalimbali na kuchangamkia fursa ya Airtel ili kupunguza tatizo idadi ya wahanga wa ukosefu wa ajira hapa nchini
Baadhi ya wajasiriamali waliohudhuria mafunzo wakiwa wamemenyoosha mkono kutaka kujibu maswali wakati wa maswali na majibu ulipowadia wakati wa hitimisho la Airtel FURSA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...