Askofu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu Dar es Salaam, Mwadhama Polycap Kadinali Pengo (kushoto), akizungumza kuhusiana na kampeni ya siku 16 za kupambana na ukatili wa kijinsia na waandishi wa habari na wanasheria wa Kituo cha Msaada wa Kisheria (WLAC), nyumbani kwake, Kurasini Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Picha na Joseph Zablon.
Wakati Tanzania kesho inazindua kampeni ya kuzuia ukatili wa kijinsia, Askofu wa Kanisa Katoliki, Jimbo
Kuu Dar es Salam, Mwadhama, Polycarp Kadinali Pengo amedai kuwa sheria dhidi ya makosa hayo zina
walakini ambao unahitaji kufanyiwa marekebisho ili kumlinda mtoto wa kike.
Pengo alisema licha ya sheria lakini pia mila na desturi zinachangia hali hiyo hivyo ni wajibu wa jamii
kubadilika na kuzikataa taratibu zote ambazo zinaondoa usawa wa kijinsia kwa wanajamii hususan katika
masuala ya elimu.
Pengo akizungumzia msimamo wa kanisa kuhusiana na vitendoa vya ukatili kwa wanawake wakati
alipotembelewa na Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake (WLAC) nyumbani kwake Kurasini, Dar
es Salaam juzi, Pengo alisema ukatili ni dhambi.
Alisema sheria zilizopo ambazo zimrungwa kuweza kuzuia vitendo hivyo vya ukatili kwa wanawake
hazijitoshelezi na zina walakini mkubwa na alitoa mfano inapotokea mtoto wa kike anapopata ujaozito,
anakuzwa shule basi na yule wa kiume nae anataka afukuzwe.
Alibainisha kuwa iwapo msichana ametakiwa kujifungua na kulea mto wake na baadae arudi shuleni basi
iwe hivyo pia kwa huyo mvulana asitishwe masomo hadi mwenzake atakapojifungua na kama aliyemtia
mimba ni mwalumu basi sheria ifuate mkondo wake.
“Kwanini tumwadibu mtoto wa kike pekee yake? Aliyemtia ujauzito yupo wapi?” alihoji na kuongeza
kuwa hata huyo msichana akirudi shule baada ya kujifungua miaka miwili aliyokaa akimlea mtoto
itamfanya arudi nyuma hatua nyingi kitaaluma.
Alisema mbaya zaidi msichana huyo ambaye wakati huo ni wazi atakuwa anasema na wadogo zake,
hataweza kuwa na utulivu wa kuweza kufuatilia masomo kama alivyokuwa awali jambo ambalo ni
sehemu ya vitendo vya ukatili wa jinsia.
Pengo alisema kipindi hiki cha maadhimisho kuelekea kilele chake Novemba 28 mwaka huu kuna haja
kubwa ya jamii kujitafakari na kuchukua hatua kukomesha mambo hayo ambayo ni inyume na mapenzi
ya Mungu na kanisa katoliki.
Alisema mila na desturi ambazo zinatoa kipaumbele cha elimu na mambo mengine kwa mtoto wa kiume
kuliko wa kike kwani ni mambo ambayo yamepitwa na wakati na hayana nafasi katika ulimwengu wa
sasa.
Awali akizungumza wakati wa mkutano huo, Mwanasheria wa WLAC, Asimwe Kabanywanyi alisema
zinduzi wa maadhimisho ayo utafanyika leo Jumatatu na kampeni za upinga hali hiyo zitaendelea nchi
nzima na kilele ni Novemba 28 Mwembeyanga, Temeke ijini Dar es Salaam na kauli mbiu ya mwaka huu
‘Amani nyumbani, duniani elimu sawa kwa wote.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...