Kijana Iddy Abdallah Chilumba, akionyesha baadhi ya bidhaa zake
anazotengeneza na kuziuza baada ya kuwezeshwa na Airtel Kupitia mpango
wake wa Airtel Fursa Tunakuwezesha .Misaada hiyo ikiwemo mashine ya
kubangulia korosho, meza maalum kwa kazi hiyo, vifaa mbalimbali na pikipiki
mpya inayomrahisishia katika nyanja ya usambazaji wa bidhaa hizo.
Airtel Tanzania imejikita katika safari ya
kuwezesha vijana hapa nchini na kuweza kubadili maisha yao kupitia nyanja
ya ujasiriamali kupitia mradi wake wa “*Airtel FURSA Tunakuwezesha”*. Ndani
ya miezi minne Airtel imeweza kufikia vijana wapatao 1,500 katika maeneo
mbalimbali hapa nchini kwa utoaji wa elimu ya ujasiriamali na misaada
mbalimbali ya kuwawezesha vijana kwa kufikia ndoto zao kupitia Airtel
Fursa. Miongoni mwa vijana hawa ni Iddy Abdallah Chilumba, mmiliki wa
biashasra ya korosho ,mwenye mri wa miaka 24 na makazi wa mjini Mtwara.
Iddy alitamani kuendesha biashara ya korosho toka akiwa na umri wa miaka
mdogo. Hata hivyo, kama vijana wengi wa Tanzania hakuweza kuwa na mtaji wa
kutosha kama moja ya changamoto aliyokabiliana nayo.Akiwa na elimu ya
kidato cha nne na stadi za msingi za kompyuta, aliweza kupata kazi ya kuuza
duka katika steshenari mkoani Mtwara ili aweze kuisaidia familia yake na
kuweza kuhifadhi kiasi kidogo cha fedha na kufanikiwa kuanzisha biashara
yake.
Kwa mtaji mdogo sana, vitendea kazi duni na ujuzi mdogo katika
usindikaji wa korosho, Iddy alijiunga na kikundi cha wanawake waliopata
udhamini kutoka SIDO. Kwa uadilifu wake na misingi bora ya ujana, kundi
hilo la wanawake lilimchukua na kufanya nae kazi kama mmoja wao na aliweza
kujifunza mambo mengi kutoka katika kikundi hicho. Pamoja na kuwa na mtaji
mdogo wa biashara, baada ya muda alianzisha biashara yake mwenyewe. Licha
ya kuchukua hatua hii ya kwanza na muhimu kuelekea ndoto yake, Iddy bado
alikuwa anakabiliwa na changamoto kubwa kama vifaa vya kufanyia kazi na
usafiri wa kusambazia bidhaa zake. Changamoto hizi zilifanya uzalishaji wa
bidhaa yake kuwa ya gharama ya juu sana kwani ilibidi kwenda kulipia kwa
ajili ya usindikaji na usafirishaji. Ndipo aliposikia *Airtel FURSA* na
kuchangamkia hiyo fursa.
*Airtel FURSA Tunakuwezesha* imeweza kubadili maisha yangu Iddi
alisema"mpaka hapa nilipofikia nimeweza kukumbana na changamoto nyingi.
Nilimpoteza baba yangu nikiwa na umri mdogo sana na nikiwa wa kwanza
kuzaliwa hivyo kuchukua majujukumu yote ya familia. Hivyo ilinibidi
kukatisha masomo yangu na kuanza kusaidia famila yangu. Siku zote nilikuwa
na ndoto za kumiliki biashara yangu mwenyewe ya korosho .Kwa hiyo nikaanza
kidogo kidogo na leo hii nawashukuru Airtel kwa kuniona na kuweza
kuniwezsha na kuweza kubadili maisha yangu. Kabya ya hapo nilikuwa napata
ugumu wa kupata wateja lakini kutokana na *Airtel FURSA* nimeweza kuongeza
mauzo yangu kwa asilimia 55% na usambazaji wa bidhaa zangu umeongezeka kwa
hali ya juu sana kwani sina tatizo la usafiri pale ninaposambaza biashara
zangu. Vile vile nimeweza kuwapatia vijana wenzangu ajira kwani nimeweza
kuajiri watu wawili ambao wanafanya kazi na mimi katika hii biashara yangu.
aliongeza, Chillumba.
Airtel inaamini katika kuwezesha vijana ili waweze kujikomboa na umasikini
kwa kuweza kujiari wao wenyewe. Kwa kuwatambua na kuwazawadia vijana ambao
wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii na kuleta mafanikio katika jamii zao.
Airtel inatimiza ahadi yake kwa kuwawezesha vijana kutimiza ndoto zao za
kujikomboa kiuchumi kwa kujiendeleza wao wenyewe na kuinua wenzao. Airtel
inaamini kwmba kwa kumuwezesha kijana katika dunia hii, unamsaidia yeye na
jamii inayomzunguka kwa kuleta maendeleo katika jamii hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...