meiomosi-2013Nawasalimuni nyote katika jina la nchi yetu nzuri Tanzania, Jina ambalo huko nyuma sote tuliliimba “Tazama ramani utaona nchi nzuri, yenye mito na mabonde mengi ya nafaka…nchi hiyo mashuhuri huitwa Tanzaniaaa!” Hakika wimbo huu vijana wengi siku hizi wanashindwa kuuimba, kwa nini? Uzuri wa taifa lao haupo tena, umepotezwa na baadhi yenu watumishi wa umma wasio na uadilifu. 

Sio siri vijana wetu kwa muda mrefu wameshindwa kujivunia taifa lao, wameshindwa kuongea mbele za watu kwa sauti kubwa kwamba wao ni Watanzania, uzuri wa taifa lao na sifa nzuri ya nchi yao imeharibiwa na vitendo kama ufisadi uliokithiri ambao umesababisha wachache katika taifa kunufaika huku wengi wakiteseka. 

Ndugu zangu watumishi wa umma, Ni kwa kupitia jina la nchi hii ndiyo leo nawaandikieni, kuwakumbusha juu ya wajibu wenu ambao kwa muda mrefu sana umekuwa hautimizwi ipasavyo! Kwanza kabisa niseme wazi kwamba nayafahamu mateso yenu, nayafahamu mahangaiko yenu ya maisha magumu, ambayo wakati mwingine yamefanya uaminifu wenu kutikiswa. Pamoja na hayo yote nasema hakuna jambo hata moja linalohalalisha kwenu ninyi kupoteza vigezo vitano muhimu vya utumishi wa umma ambavyo ni; 

1.UADILIFU 
2.UAMINIFU 
3.KUSEMA KWELI DAIMA 
4.UZALENDO NA DHAMIRA 
5.HOFU YA MUNGU. 

Yeyote kati yenu aliyehalalisha kuondoka kwa vitu vitano nilivyovitaja hapo juu kwa sababu ya aidha kipato kidogo anachokipata serikalini, akavunjika moyo na kuacha kuwatumikia wananchi, ama akachagua kuendeleza rushwa na kukosa uzalendo, huyu hatufai kuwa mtumishi wa umma. 

SOMA ZAIDI HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. 20 miaka iliyopita hata wewe hukuandika hivi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...