Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi inayowakabili watuhumiwa kumi (10) wa ujambazi wanaodaiwa kufanya mauaji ya Askari Polisi wa kituo Stakishari jijini Dar es Salaam.
Watuhumiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka saba likiwamo la mauaji ya askari wa kituo cha polisi Stakishari kilichopo Manispaa ya Ilala.

Upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali Peter Njike ulidai mahakamani hapo kuwa watuhumiwa hao wanadaiwa kufanya kosa hilo Julai 12 mwaka huu kinyume na kifungu cha 196 cha sheria cha adhabu ya sura 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Ulidai kuwa, upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. Watuhumiwa hao walirudishwa rumande kwa sababu mashtaka hayo hayana dhamana. Hata hivyo, Hakimu Simba alihairisha kesi hiyo hadi Desemba 10 mwaka huu itakapotajwa tena. 
Watuhumiwa wanaodaiwa kufanya mauaji ya Askari wa Kituo cha Stakishari ni Omary makota(28),Rajab Ulatule(22),Ramadhani Ulatule(20),Fadhiri Lukwembe(23),Ally Salum(63).
Wengine ni Hamis Salum(51),Nassoro Abdalah(42)Seleman Salum(83),Said Mohamed(67) na Said Abdulah(45). Watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani hapo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kwa ajili ya kutajwa. 
Awali, watuhumiwa hao wanadaiwa kuvamia kituo cha polisi stakishari na kuwaua askari namba D 6952 Sajenti Adam, E 3962 Koplo Gaudin,E 1279,koplo Peter na G3010,PC Anthony.
Wengine waliouawa katika tukio hilo ni pamoja na Salehe Semkoko, Erick Swai na Jackline Duma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...