
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa matamasha ya muziki wa injili nchini Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam wakati alipofafanua mambo mbalimbali kuhusu maandalizi ya tamasha la kushukuru baada ya kufanyika na kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa Tanzania salama salimini.
Msama amesema maandalizi
yanaendelea vizuri na amemtangaza rasmi mwimbaji Rose Muhando kama mmoja
wa waimbaji wa muziki wa injili watakaoshiriki katika tamasha hilo,
linalotarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Desemba 25 na
kushirikisha waimbaji wa kimataifa kutoka nchi za Afrika na Ulaya,
ambapo ameongeza kwamba mazungumzo bado yanaendelea na waimbaji wengine
kutoka nje ya nchi.
Katika picha katikati ni Mwimbaji
wa muziki wa Injili Rose Muhando akishiriki katika mkutano huo na
kushoto ni William Kapawaga mmoja wa waratibu wa Tamasha hilo kutoka
Kampuni ya Msama Promotion.


Mwimbaji
wa muziki wa Injili Rose Muhando akiwaelezea waandishi wa habari jinsi
alivyojiandaa kutumbuiza katika tamasha hilo la kushukuru, Kulia ni
Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama.
baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion wakati alipokuwa akizungumza nao jijini Dar es salaam kuhusiana na Tamasha hilo.
baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion wakati alipokuwa akizungumza nao jijini Dar es salaam kuhusiana na Tamasha hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...