Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya Freconic Ideaz, imeandaa tamasha la burudani la ‘Instagram party’ litakalofanyika kesho kutwa kwenye Ukumbi wa Escape One Mikocheni jijini Dar es Salaam likiwa na lengo la kuwakumbusha wapenzi wa muziki, mavazi na misemo ya kizamani.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Freconic Ideaz, Fred Ngimba alisema pia tamasha hilo litahusisha watu wenye ushawishi mkubwa katika mitandao ya kijamii na wasanii mbalimbali wa muziki na filamu wanamichezo na wanasiasa na kuweza kufanikisha mashabiki wao kuweza kupiga nao picha katika red carpert.
Alisema wadau na marafiki mbalimbali wanaotumia mitandao ya kijamii watakutana siku hiyo kuweza kufahamiana na kubadilishana mawazo huku wakipata burudani mbalimbali.
“Kiingilio katika tamasha hili kitakuwa ni sh. 50,000 kwa viti maalumu na vile vya kawaida ni sh. 10,000, ambapo halitaishia hapa ila litaendelea katika Mikoa ya Mwanza, Morogoro, Tanga, Dodoma na Iringa,” alisema Ngimba.
Alitoa mwito kwa wadau wa muziki wa mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi kushuhudia burudani itakayotolewa siku hiyo kwani kuna maboresho makubwa yamefanyika katika kuongeza ubunifu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Freconic ideaz, Fred Ngimba akifafanua jambo alipokuwa anaongea na waandishi wa habari jana katika fukwe za Escape One kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya tamasha kubwa la burudani litakalofanyika jumamosi hii tarehe 28 ,kulia kwake ni Meneja mawasaliano wa Freconic ideaz Krantz Mwantepele.
Mmoja wa wadau akitembelea ukurasa wa INSTAGRAM PART TZ kupata taarifa mbalimbali kuhusu tamasha hili litakalowakumbusha wapenzi wa burudani nyimbo za zamani ,misemo ya zamani hata mavazi ya zamani kukiwa na kauli mbiu ya BONGO THROW BACK.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...