Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitoa taarifa rasmi ya Serikali kuhusu vifungu vya sheria   juu ya uhalali wa kuendelea kuwepo madarakani Rais wa Zanzibar.
Na Othman Khamis Ame, OMPR
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imewahakikishia Wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kwamba Rais aliyepo madarakani hivi sasa ataendelea kushika madaraka ya Urais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi mpaka pale utaratibu wa Kikatiba na Kisheria wa kumpata Rais utakapokamilika.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akitoa Taarifa ya Serikali akisisitiza Taarifa ya awali ya Serikali iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuhusiana na kauli za kupotosha zinazotolewa na baadhi ya Viongozi wa vyama vya Kisiasa kuhusu uhalali wa kuendelea kuwepo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliyopo madarakani pamoja na Serikali yake.
Balozi Seif aliwaomba Wananchi wazipuuze kauli za upotoshaji zinazotolewa zikiashira zaidi uvunjifu wa amani na kuwataka waendee kuwa watulivu na kudumisha amani iliyopo Nchini.
Alisema Kifungu cha 28 Mbili {a} cha Katiba ambacho kimekuwa kikitumika katika kutoa tafrisi potofu kwa Wananchi  kwamba Rais aliyopo madarakani atamaliza muda wake wa miaka mitano kuanzia Tarehe ambayo alipokula kiapo cha uaminifu na kiapo cha kuwa Rais.
Balozi Seif alieleza kwamba ni dhahiri kwamba dhamira ya kifungu hicho cha Katiba ilikuwa kuweka bayana kuwa kama uchaguzi Mkuu utafanyika na msindi wa kiti chja Urais atatangazwa rasmi na Tumen ys Uchaguzi, hivyo muda wake wa kuendelea Mtu kuwa Rais ungemalizika kwa kufuatana na masharti ya Kifungu hicho.
Alifafanua kwa kuwa Tume ya Uchaguzi haikumtangaza mshindi wa kiti cha nafasi ya Urais ni dhahiri masharti ya kifungu hicho hayataweza kusimama na hivyo masharti ya Kifungu cha 28 {1} {a} cha Katiba kitakuwa na nguvu za Kikatiba kumpa uwezo wa Rais aliyopo madarakani kuendelea na madaraka ya Urais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Alisema Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi anapatikana  kwa mujibu wa masharti ya Kifungu cha 27 cha Katiba ambacho Rais anachaguliwa kufuatana na Katiba Hiyo na kwa mujibu wa Sheria yoyote itakayotungwa na Baraza la Wawakilishi hukusu Uchaguzi wa Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Balozi Seif alifahamisha kuwa ili Rais wa Zanzibar apatikane kwa mujibu wa Katiba na sheria ya Uchaguzi nambari 11 ya Mwaka 1984, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar inapaswa kuendesha uchaguzi na hatimae kumtangaza mshindi wa nafasi ya Urais ambae atashika madaraka hayo pale ambapo atakuwa ameapishwa rasmi kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Katiba ya Zanzibar.
Alisema Kifungu cha 28 {1} {a} cha Katiba kinaweka utaratibu kuhusu muda wa kuendelea kuwa kuwa Rais, na kwamba kwa kufuatana na kifungu hicho, mtu aliyechaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ataendelea na dhamana hiyo mpaka pale ambapo Rais anayefuata ale kiapo cha kuwa Rais.
Alieleza kwamba kwa msingi huo wa Kikatiba ni vyema Wananchi wakafahamu na kuelewa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Braza la Mapinduzi ataendelea kuwepo madarakani mkapa pale Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar itakapomtangaza mshindi wa kiti cha Urais na Rais Mteule atashika madaraka hayo baada ya kuapishwa rasmi kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Katiba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Katika hadith quds, M.Mungu anamwambia baba yetu Adam achukue kila katika 1000, mtoto 1 aende nao kwenye bustani la milele. Kuna mafunzo makubwa katika habari hii. Nikijihukumu, mimi naweza kuwa ni miongoni mwa 999 watakaoachwa kwani mimi si msafi wa matendo, na nnavyoona matukio sasa hivi duniani sishangai naona 998 wa kuungana nami wanapatikana kirahisi. Swali, kwa nini Adam akuchague wewe?

    Binadamu wa sasa humuadhibu mtu ati kwa sababu baba yake alimdhulum. Naona kwa nini Nelson Mandela alijaaliwa hekima. Pamoja na kufungwa miaka mingi, alivyotoka gerezani, alisamehe makaburu. Angetaka kuwafanya kama Idi Amin au Mugabe angeweza.

    Tanzania inaanza kushindwa uongozi wa bara la afrika kwa kuanza kutafuta kuwa mfano mbaya. Kama vile Misri. Walikuwa mfano mzuri, sasa hivi ni wabaya kuliko woote. Demokrasia ni kumvumilia atawale usiyempenda mradi kachaguliwa. Kazi yako ni kumuailisha na kupiga kampeni uli asichaguliwe tena.

    ReplyDelete
  2. Mpaka pale patapokuwepo na sheria ya kuadhibu wabaguzi, sisi bado ni wachanga. kulaani ubaguzi bila adhabu yamaanisha ubaguzi ni kosa tuu lakini halistahili adhabu.

    Naanza kuona kwa nini Tanzania haina adhabu ya ubaguzi. We ride it sometimes. We reserved it for those times.

    ReplyDelete
  3. It's shame!..
    Na inatia hasira sana,
    Ushauri; ni bora mgawane kwani visiwa viwili hivyo na kuepushana kutumia nguvu sana kujieleza na ili muishi kwa Amani, wapinzani wasiwasumbue. Kwani mambo yako wazi!!

    ReplyDelete
  4. Tanzania nchi yangu nikionacho hapa ni undumilakuwili ambao ulijificha muda mrefu na watu wakahisi kuwa tunafuata demokrasia ambayo waliotuletea walikuwa na maana yao ambayo hatukuijua uthabiti wake.Naiona Tanzania ya miaka 20 ijayo kuwa ya mabadiliko ya kujitengeneza bila kuhofia vitisho wala nguvu ya wapinga maendeleo wanaojinadi kuwa wapenda maendeleo.

    ReplyDelete
  5. 'It is enough that the people know there was an election. The people who cast the votes decide nothing. The people who count the votes decide everything.'
    --Joseph Stalin

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...