Mdau Krantz Mwantepele akizungumza na Raia waamilifu kutoka kijiji cha Kilago wilayani Kahama ambapo nilipata nafasi ya kujua mambo mbalimbali ikwemo mchango wa uraghabishi katika kijiji hicho katika sekta ya elimu 

Na Krantz Mwantepele , Kahama

Utoro ni tabia ya kuondoka au kutokufika mahali mara kwa mara bila ya kutoa taarifa. Tabia hii ipo kwenye maeneo ya makazini pamoja na shuleni. Katika baadhi ya kata za wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga. 

Tabia hii imekuwa kero kwa wanajamii wa kata za Nyandekwa na Kilago kwa kuwa inawarudisha nyuma kimaendeleo. Wakiwa kama sehemu ya wananchi wa kata hizo, waraghbishi wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha watoto watoro wanahudhuria shuleni.

Ikiwa kama sehemu ya uraghbishi, kutambua changamoto zinazokabili jamii wanayoishi, waraghbishi walitambua kwamba hili ni tatizo na hivyo kuamua kulishughulikia. 

“Nikiwa njiani kuelekea kwenye shughuli zangu, nikakuta watoto wamejibanza kwenye kichaka, na wengine walikuwa wakicheza mpira. Nikataka kujua kulikoni mbona hawapo shuleni, wakati ni muda wa masomo?”

Hili ni swali ambalo raia mwamilifu na mraghbishi Paul Izengo toka katika kijiji cha Nyandekwa kilichopo wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, alitaka kulipatia majibu yake. Udadisi huu ndio uliopelekea kwa yeye kuwasogelea watoto ambao kimsingi walitakiwa kuwa shuleni mda huo na kutaka kujua kulikoni.

Raia Waamilifu, Mathew Charles (kushoto) wa kijiji cha Kilago na Alphonce Peter toka kijiji cha Ufala wilayani Kahama wakifurahia jambo walipkuwa wakijadili tatizo la utoro mashuleni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...