Idadi ya Raia wa kigeni kutoka nchini Ephiopia waliokuwa wakisafirishwa na Gari la magazeti la kampuni ya Mwananchi Communication Ltd yafikia 12 baada ya wengine 4 kukamatwa Jioni wakiwa Eneo la Kibwabwa mjini Iringa wakiwa wamefichwa porini.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Iringa Peter Kakamba amesema kuwa tayari ametuma usafiri kwenda kuwabeba Raia hao ambao wanadai walishushwa katika gari hilo aina ya Hiace ili kuvuka eneo la ukaguzi wa Magari ( check pointi) kijiji cha Igumbilo nje kidogo ya mji wa Iringa.
Wakati huo huo Kampuni ya Mwananchi Communication Limited (MCL) imetoa ufafanuzi kuhusiana na kuhusishwa na kadhia hiyo. Soma zaidi:
Wakati huo huo Kampuni ya Mwananchi Communication Limited (MCL) imetoa ufafanuzi kuhusiana na kuhusishwa na kadhia hiyo. Soma zaidi:
Kufuatana na taarifa ya Jeshi la polisi mkoa wa Iringa kukamata gari la kampuni ya Okanda lenye usajili namba T745 DED Toyota Hiace inayosafirisha magazeti ya MCL jana tarehe 27 Januari 2016 asubuhi likiwa linadaiwa kubeba WAHAMIAJI HARAMU. Tunapenda kutoa maelezo yafuatayo:
• MCL haijawahi kufanya, haifanyi na hivyo haihusiki kwa hali yoyote katika tukio hili. Watuhumiwa (madereva) wanaodaiwa kuhuhusika na tukio hili si wafanyakazi wa Mwananchi Communications Limited bali ni wa Okanda kampuni ambayo imeingia kandarasi na MCL kusafirisha magazeti yake kutoka Dar es Salaam kwenda Mbeya
• MCL itaendelea kufanya kazi za biashara yetu ya habari kwa uadilifu na weledi wa hali ya juu.
• MCL inaangalia uwezekano wa kuchukua hatua kali zaidi dhidi ya mkandarasi ikiwepo kusitisha mkataba.
• Tunawapa pole wasomaji wetu wote na umma kwa ujumla kwa usumbufu mlioupata kutokana na habari za tukio hili
Francis Nanai
Mkurugenzi Mtendaji – MCL



Kama ni kweli Taasisi za Ulinzi mnayafanyiakazi maoni yetu, basi sisi raia wema tunaomba wahusika wawajibishwe ipasavyo. Nchi hii ni yetu na wachache wasijinufaishe kwa biashara haramu na hujuma kwa Taifa. Hawa niwahujumuwa Taifa na wanatuhujumu Watanzania katika juhudi zetu za pamoja. Kila Mtanzaniana iila aliyepo Tanzania ni lazima afanyekazi halali na si haramu kama hii. Tunaomba mtandao huu wa jamii lenegsha maoni haya kwa wahusika na hawa wapendao kujinufaisha kwa haramu wakomeshwe. Tunataka heshima ya Taifa letu na kwa Watanzani kwa ujumla.
ReplyDelete