Huu ni uchambuzi wa Habari toka vituo mbalimbali vya Televisheni January 27, 2016.
Serikali imetolea ufafanuzi kuhusu uamuzi wa kutorusha matangazo ya moja kwa moja ya majadiliano ya Bunge.
Serikali imetolea ufafanuzi kuhusu uamuzi wa kutorusha matangazo ya moja kwa moja ya majadiliano ya Bunge.


cha msingi wakubali kwamba nchi imeshapinduka upande wa pili. Watanzania wa leo sio wa jana, wanahitaji vitu Live sio kurekodiwa.
ReplyDeleteMbona 99% ya yale unayoonyeshwa kwenye tv sio Live?iwe ni taarifa ya habari au matukio mengine . kifupi, ni bora watu wakaacha kuingiza siasa kwenye kila jambo,kuna mambo mengi ya msingi katika majimbo yetu yanohitaji kutolewa maelezo na serikali nasio swali la kuwa live au recorded. Please
DeleteDemokrasia ina gharama haiwi bure. Kama mwataka wananchi wakue zaidi kidemokrasia lazima muwaruhusu wapate hapari za ufanyaji kazi wa wawakilishi wao.
ReplyDeleteMdau unamaana demokrasia inajengwa zaidi pale tu wawakilishi wao wanapokuwa "live kwenye tv"? Na haki yao hupotea wakisikizwa kwenye recorded programs?
DeleteHili nalo mbona kama lina fanana na jipu..Mwanzo TBC ndiyo kilikuwa ni chombo pekee kinachoweza kurusha Mwenendo wa Bunge ''LIVE'' huku vituo vyengine vikurusha kutoka TBC,Hilo wananchi hawakupiga kelele, leo tena hakuna kuonyesha ''LIVE" Wananchi wasubiri recorded kuanzia saa 4 usiku hadi saa 5 Usiku, muda huo huo Serikali inataka watu kuwahi makazini ukifika zaidi ya saa 2.30 asubuhi unakutana na waziri yupo mlangoni kwa nini umechelewa kuingia kazini au ukute daftari limeshapigwa mstari mwekundu anayefika baada ya mstari andike maelezo.chingine Bunge linaanza saa 3 asubuh hadi saa 7. awamu ya pili kuanzia saa 10 jion hadi saa 12 au zaidi,ni almost masaa 7 au nane halafu Mh.Nape kwa niamba ya serikali anasema bunge litarudiwa lisaa li moja? jamani tunaelekea wapi, mbona tunanyimwa haki za msingi na uhuru wa kupata habari? eeh mungu tunako elekea sasa tutaambiwa marufuku kuangalia TV sasa.huu ni mtazamo wangu tuu kwa serikali yetu mpya.
ReplyDeleteKutorusha hayo matangazo live ni uamuzi mzuri hizo fedha za matangazo zikanunulie madawa hospitali na kutoa elimu bure.
ReplyDelete