Watumishi wa Mahakama
ya Tanzania na wadau mbalimbali wa wakiingia katika viwanja vya Mnazi mmoja kwa
maandamano leo jijini Dar es salaam wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki
ya Sheria.
Watumishi wa Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), Askari wa Jeshi la Magereza na
Watumishi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) wakiwa wamebeba mabango ya
Ofisi zao wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria Nchini leo jijini Dar es salaam.
Jaji Mkuu wa Tanzania
Mhe. Mohamed Chande Othman (Mwenye T-shirt nyeupe kulia), Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam
Said Mecki Sadiki (wa Pili kulia) na Watendaji wa Mahakama ya Tanzania
wakishiriki mazoezi ya viungo ya pamoja na wadau mbalimbali wa Mahakama leo
katika viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria Nchini.
Jaji Kiongozi Mhe.
Shaban Lila (katikati) akiongoza mazoezi ya pamoja ya Wadau wa Mahakama leo
katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam wakati wa Ufunguzi wa Wiki ya Sheria nchini.
Jaji Mkuu wa Tanzania
Mhe. Mohamed Chande Othman akizungumza na wadau mbalimbali wa Mahakama waliohudhuria
Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria mwaka 2016 katika viwanja vya Mnazi mmoja leo jijini
Dar es salaam.
Baadhi ya Wanachi wakifuatilia
matukio mbalimbali wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA








Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...