Katika mwendelezo wake wa kufanya maisha ya watanzania kuwa murua na kuwapeleka katika karne ya sayansi na teknolojia, kampuni ya mawasiliano ya Vodacom leo imezindua simu ya mkononi ya gharama nafuu kabisa ambayo haijawahi kutokea nchini.
Simu hiyo  aina ya Alcatel ambayo bei yake ni nafuu ya shilingi 20,000/- imeanza kusambazwa sehemu mbalimbali nchini na itapatikana katika maduka ya Vodacom na mawakala wake wote nchini kote hususani maeneo ya vijijini.
Akiongea kuhusu uzinduzi wa simu hii mpya,Mkurugenzi Mtendaji wa  Vodacom Tanzania, Ian Ferrao alisema “Vodacom imeingiza simu hii ya gharama nafuu ambayo imetengenezwa kumuwezesha mtumiaji kupata huduma mbalimbali na dhamira yetu kubwa ni kuendelea kufanya ubunifu wa kiteknolojia wa kurahisisha maisha ya watumiaji wa simu pia kuwapeleka katika ulimwengu wa teknolojia”.Alisema.
Alisema kwa mwaka huu kampuni itaendelea kubuni huduma mbalimbali  za kurahisisha mawasiliano dhamira yake kubwa ikiwa ni kuhakikisha kila mtanzania ameunganishwa kwenye mtandao na anafurahia maisha kupitia teknolojia ya simu.
Nae Meneja wa huduma na bidhaa wa kampuni hiyo,Edwin Byampanju aliielezea simu hiyo kuwa ina uimara mkubwa, ina kioo chenye ukubwa wa inchi 2 na mwonekano wa mbele wenye rangi maridhawa,ina kamera yenye ukubwa wa MP 1.3, betri inayotunza chaji  kwa muda mrefu zaidi ya siku tano,ina redio pia inao uwezo wa kutumia kadi ya kumbukumbu hadi GB 16”.
Aliwataka wateja wote wanaotumia mtandao wa Vodacom kuchangamkia fursa ya kumiliki simu imara na yenye ubora wa kisasa kwa gharama nafuu na kuendelea kupata huduma bora zinazorahisisha maisha.
 Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu(kushoto) akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati wa  uzinduzi wa simu mpya aina ya Alcatel mwishoni mwa wiki yenye vioo 2, kamera ,radio, MP 1.3, kadi yenye GB 16 na betri  yake inayotunza chaji  kwa muda mrefu.Simu hiyo inapatikana katika maduka yote ya Vodacom nchini  kwa   Tsh.20,000 tu ,Kulia ni Meneja wa huduma na bidhaa wa kampuni hiyo,Edwin Byampanju.

Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kushoto)na Meneja wa huduma na bidhaa wa kampuni hiyo,Edwin Byampanju wakionesha simu mpya aina ya Alcatel kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa uzinduzi wa simu hiyo mwishoni mwa wiki inayopatikana kwenye maduka yote ya kampuni hiyo nchini kwa Tsh.20,000 tu.Simu hiyo ina vioo 2,kamera,radio,MP 1.3, na kadi yenye GB 16 na betri inayotunza chaji  kwa muda mrefu zaidi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...