Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wapili kushoto) akiwasili Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya kikazi. Wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Hassan Simba, kulia ni Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali, Pius Nyambacha. Katika hotuba yake, Rwegasira alilipongeza jeshi hilo kwa utendaji wa kazi mzuri na kulitaka liongeze kasi zaidi katika ukusanyaji wa mapato.
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali, Pius Nyambacha (kulia) akitoa taarifa ya utendaji wa Jeshi lake kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati) wakati Katibu Mkuu huyo alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake, Rwegasira alilipongeza jeshi hilo kwa utendaji wa kazi mzuri na kulitaka liongeze kasi zaidi katika ukusanyaji wa mapato. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Hassan Simba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...