Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Generali Gaudence Milanzi (kulia) akizungumza na viongozi wa Kundi la Washirika wa Maendeleo katika sekta ya Mazingira, Maliasili na Mabadiliko ya Tabia Nchi (Development Partners Group on Environment, Natural Resources and Climate Change (DPG-E) walipoonana leo tarehe 19 Januari, 2016 katika ukumbi wa Selous uliopo makao makuu ya Wizara hiyo Mpingo House. Kundi hilo liliomba kuonana na Katibu Mkuu huyo kwa ajili ya utambulisho na kujadili mambo muhimu ya maendeleo katika sekta hiyo.
 
Bi. Lena Thiede (kushoto) kutoka ubalozi wa Ujerumani ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Shirikisho la Kikanda Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kutoka Kundi la Washirika wa Maendeleo katika sekta ya Mazingira, Maliasili na Mabadiliko ya Tabia Nchi (DPG-E) akizungumza katika kikao hicho ambapo alielezea kazi ya Kundi hilo kuwa ni kuandaa mijadala maalum ya kisera na Serikali pamoja na wadau wengine wa maeneo husika, kuratibu miradi na mipango ya kundi hilo na kuhamasisha mawasiliano na utetezi wa pamoja baina yake na Serikali na wadau wengine katika sekta hizo. Katikati ni Bi. Clara Makenya kutoka UNEP ambaye ni Mratibu wa Kitaifa wa Kundi hilo na Bw. Steven Nyagondi Sekretarieti ya Kundi hilo. 
 
Bwana Bernad Lubogo (kulia) Afisa Mipango Wizara ya Maliasili na Utalii akichangia jambo katika kikao hicho, Wengine ni Bi. Bertha Nyange (Katikati) Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mipango na Bw. Joseph Sendwa Afisa Utalii Wizara ya Maliasili na Utalii.
Baadhi ya washiriki wa kikao hicho kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.
(Picha na Hamza Temba - Kitengo cha Mawasiliano Serikalini - Wizara ya Maliasili na Utalii)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...