Na Bashir  Yakub. 

Hakimiliki  katika  masuala  ya  ardhi  huhusisha  umiliki  wa ardhi  zenye hati. Umiliki huu  hutoa  wajibu  na haki  fulani  kwa mmiliki  katika  ardhi husika. Si  rahisi  kudai  una  hakimiliki  katika  ardhi kama  hauna  hati.  

Aidha  tumezoea  kuona  hati  zilizo  na  jina  la  mtu  mmoja mmoja. Hii  ni  hata  kwa  wanandoa ambao  hudai   mali  husika zinatokana  na  jasho lao wote. Lakini  je  unajua  kuwa  inawezekana   hati miliki  ikawa  na  majina  ya wanandoa  wote  badala  ya  kuwa  na  jina la mmoja tu hasa   baba   ambao  ndio  wengi  hupenda  majina  yao  yaonekane  hapo ?.  Jambo  hili  linawezekana na  linaruhusiwa.

1.HAKIMILIKI  YA  PAMOJA  KUONDOA  MGOGORO.
Kutokuelewana  ambako  mara  kadhaa  hutokea  baada  ya  kifo  cha  mmoja  wa  wanandoa  kwaweza   kuondolewa  na  umiliki  wa  ardhi  wa  pamoja. Ikiwa una  wasiwasi  juu  ya  mustakabali  wa  mali  hasa  ardhi  huko  mbeleni  ni  vema  basi  ukachukua  hatua  hii  ya  kusajili  kwa umiliki  wa  pamoja. 
Kama kiwanja/ nyumba  ina  hati  yenye majina mawili  la baba na  mama halafu mmoja  wao  akafariki itakuwa   ni  vigumu  ndugu  au  mwingine  yeyote  mwenye  nia  mbaya kudai  umiliki  wa kiwanja/nyumba hiyo. 

Lakini hali  itakuwa  tofauti iwapo  hati  ina  jina  la  mmoja  na  huyohuyo mmoja  ndiye  aliyefariki. Pale  pote  ambapo  ndugu  walidhulumu  mali  za  marehemu  hasa  ardhi  ni  pale  ambapo  kuna jina  la mmoja.

Mara  nyingi  fitina  huingia pale penye  mwanya  wa  kufanya  hivyo. Si  rahisi  fitina kuingia  pasi na  mwanya. Kuweka majina  ya  wanandoa wote  kwenye  hati  za  ardhi  ni  hatua  ya  kuziba  mwanya  wa  fitina. Itawezekanaje  ndugu au mwingine  mwenye  nia  ovu kudai umiliki  wa  ardhi  ya  marehemu huku  akijua  kuwa  hati   inalo  jina  la  mke  pia.  Si  rahisi  hata   kidogo. 

Lakini  pia  umiliki  wa  pamoja  huondoa  mgogoro  pale  panapo  talaka. Swali  la  je  mwanandoa  fulani  amechangia  chochote  katika  kupatikana  kwa  mali  huwa  halipo  ikiwa  majina  yote  mawili  ya  wanandoa  yameonekana  kwenye  hati. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. asante kwa kutuelimisha Mungu akubariki, mara nyingi watanzania tunaishi kwa mazoea, elimu hii itawafungua wengi macho!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...