Na Bashir Yakub .
Kupitia makala haya wako Watanzania ambao wanao marafiki wa kigeni, wanao wafanyabiashara wenzao wa kigeni, ndugu wa kigeni, na wengine wanahisa wenzao katika makampuni mbalimbali ambao wangependa wenzao hao wapate ardhi ya uwekezaji Tanzania. Makala haya ni nafasi kwao kujua mambo ya msingi ya awali kuhusu namna ya kupata ardhi kwa hao wageni.
Aidha mara kadhaa makala yetu yameeleza taratibu mbalimbali ambazo Mtanzania huweza kupitia ili kupata haki ya kumiliki ardhi. Sanjari na hilo imeelezwa mara nyingi pia namna nzuri ya kuweza kupata ardhi huku ukiepuka migogoro ambayo huwaingiza wengi katika hasara ikiwa ni pamoja na kuwapotezea muda.
Iliwahi kuelezwa hapa kuwa Mtanzania anaweza kupata ardhi kwa kununua, kurithi, kuzawadiwa, njia ya fidia, na kwa kutwaa eneo lisilo na mmiliki.
Hii ni kwa raia wa Tanzania. Yumkini raia wasio watanzania nao wanazo haki zao katika ardhi yetu. Raia wasio Watanzania wanaweza kupatiwa ardhi kwa ajili ya matumizi. Kubwa kwao hupatiwa ardhi kwa ajili ya uwekezaji kwa manufaa ya taifa.
Kupitia hili zipo namna tano ambazo raia wasio Watanzania wanaweza kupitia hadi kupatiwa ardhi.
1.SHERIA ZINAZOWARUHUSU WAGENI KUPATIWA ARDHI.
Sheria kuu inayowaruhusu raia wa kigeni kupatiwa ardhi nchini ni sheria namba 4 sheria ya ardhi ya mwaka 1999. Kifungu cha 19( 2 ) cha sheria hii kinasema kuwa mtu au kikundi cha watu ambacho kimejiunga kama kampuni au bila kampuni ambacho wahusika wake ni raia wa kigeni wanaweza kupata haki ya kumiliki ardhi kwa ajili ya uwekezaji.
Sheria nyingine inayotoa mwongozo kwa raia wa kigeni kupata ardhi Tanzania ni sura ya 38 sheria ya uwekezaji ya mwaka 1997. Sheria hii hueleza namna ya kumpatia mwekezaji ardhi, matumizi, na muda wa mwekezaji mgeni kutumia ardhi hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...