Mkuu wa Idara ya Huduma ya Wagonjwa wa nje toka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Raymond Mwenesano akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari leo jijini Dara es salaam kuhusu utaratibu mpya wa utoaji wa Huduma kwa wagonjwa wa nje ambapo huduma zitakuwa zikitolewa kuanzia Jumatatu hadi jumamosi ikiwa ni moja ya mikakati ya Hosipitali hiyo kuboresha huduma zake kwa wananchi.
Afisa Uhusiano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Bi Neema Mwangomo akizungumza leo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano na Vyombo vya habari amabapo aliwataka Watanzania kutumia huduma zinazotolewa na Hospitali hiyo ya Taifa kwa kuwa inao wataalamu wakutosha kutimiza jukumu hilo la kuwahudumia wananchi.
Mkuu wa Idara ya Huduma ya Wagonjwa wa nje toka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Raymond Mwenesano akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano ulioenga kueleza mikakati ya Hosipitai hiyo katika kuboresha huduma zake kwa wananchi.kushoto ni Afisa Uhusiano wa Hospitali hiyo Bi Neema Mwangomo na kushoto ni Muuguzi wa Hospitali hiyo Bi June Samwel.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...