RAIS mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, tarehe 19 Januari, 2016 alihani msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi S.S. Suleiman aliyefariki wakati akifanya mazoezi ya kuogelea Tanganyika Swimminga Club maeneo ya Feri- Kigamboni- Dar es Salaam tarehe 18 Januari, 2016 alfajiri.

Rais Kikwete na mkewe, Mama Salma Kikwete waliwasili nyumbani kwa marehemu Upanga jana saa 10.30 jioni na kulakiwa na  mdogo wa marehemu, Mhandisi Nassir Said Suleiman na wanafamilia wengine akiwemo Naibu Waziri wa zamani wa Mawasiliano na Uchukuzi, Dk. Maua Daftari.

 Pia alilakiwa na viongozi wa TAA, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu (DHRA), Bw.  Laurent Mwigune, Mwanasheria Mkuu wa TAA, Wakili  Ramadhan Maleta na Meneja Mwandamizi wa Utawala na Raslimali Watu, Mohammed Ally.

Baada ya kulakiwa, alikwenda moja kwa moja kuweka saini katika kitabu cha maombolezo kisha kutoa mkono wa pole kwa wanafamilia, mdogo wa marehemu, Mhandisi Nassir, watoto wa marehemu, Mohammed, Said na Hossam, mama mzazi wa marehemu, ndugu, jamaa na marafiki na viongozi wa TAA.

 Katika rambirambi zake, Rais Mstaafu, Dkt. Kikwete alisema alipokea kwa mshituko mkubwa akiwa kijijini kwake Msoga, Chalinze, habari za kifo cha Mhandisi Suleiman na hakuamini hadi alipopata ujumbe rasmi wa simu baada ya kuulizia zaidi.

SOMA ZAIDI HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...