Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imepokea msaada wa mashine moja ya kumsaidia mtoto kupumua Ventilator Machine yenye thamani ya Shilingi Milioni 17.
Msaada huo umetolewa na Human Walfare Trust kwa ajili ya Idara ya magonjwa ya dharura na ajali katika hospitali ya Taifa Muhimbili.
Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya Human Walfare Trust , Bwana Dipak Vassa amesema lengo ni kuendelea kusaidia sekta ya afya mbapo wanataraji kuipanua zaidi idara ya magonjwa ya dharura na ajali kwenye hospitali hiyo.
Mipango mingine ni kutengeneza uwanja maalumu wa kuchezea ili watoto wenye matatizo ya Saratani ambao wanapatiwa matibabu MNH wautumie uwanja huo na pia kutoa usafiri wa basi kwa ajili ya kuwapeleka Ocean Road.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Mseru amewashukuru Human Walfare Trust kwa msaada huo na kuahidi kuutumia vema kwa lengo lililokusudiwa.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Mseru akipokea msaada wa mashine ya kuwasaidia watoto kupumua ambayo imetolewa na Human Walfare Trust kwa ajili ya Idara ya Magonjwa ya Dharua na Ajali hapa MNH.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Mseru akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakuu wa Idara na wawakilishi kutoka Human Walfare Trust ambao wametoa msaada wa mashine ya kusaidia watoto kupumua (Ventilator Machine).
Picha kwa Niaba ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...