Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya, (kushoto) akisalimiana na
maafisa wa Jeshi la Magereza alipotembelea Gereza la uzalishaji mifugo Mtego wa
Simba lililopo Kingolwira mkoani Morogoro.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya, akisaini kitabu cha wageni mara
baada ya kuwasili katika Gereza la uzalishaji mifugo Mtego wa Simba mkoani
Morogoro. Kulia ni Mkuu wa Gereza hilo Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Omari
Msepwa.
Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la
Magereza katika shamba la uzalishaji mifugo Gereza la Mtego wa Simba, Constatus
Magori akitoa maelezo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto) alipotembelea Gereza hilo Januari 30, 2016 kujionea
shughuli mbalimbali za uzalishaji zinazofanywa gerezani hapo mkoani Morogoro.
Kundi la ng’ombe wa maziwa
wanaofugwa katika shamba la uzalishaji mifugo Gereza la Mtego wa Simba,
Kingolwira mkoani Morogoro wakiwa malishoni kama wanavyoonekana katika picha.
Mtaalamu wa mifugo katika
mradi wa ufugaji kuku wa mayai na nyama uliopo Gereza Kuu la Wanawake Tanzania,
lililopo Kingolwira mkoani Morogoro, Sajenti Sarah Kabunda (wapili kushoto) akitoa
maelezo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba
Yahya (kushoto) alipotembelea Gereza hilo Januari 30, 2016 kujionea shughuli
mbalimbali za uzalishaji zinazofanywa
gerezani hapo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (wa pili kushoto), akiangalia
moja ya mashuka yanayofumwa kwa ustadi mkubwa na wafungwa wa kike katika Gereza
Kuu la Wanawake Tanzania, Kingolwira mkoani Morogoro. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi).


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...