DR. ELIEZER KWEGRY FINEHAS CHIDUO
09/09/1950  -  26/12/2015   

 Familia ya Marehemu Dr Eliezer Finehas Chiduo wa Chuo kikuu cha Dsm wanapenda kutoa shukrani zao za dhati kwa wote walioshirikiana nao kwa namna moja au nyingine kwenye kipindi kigumu cha msiba na kuhitimisha safari ya mwisho ya baba yao  mpendwa  Dr Eliezer Finehas  Chiduo kilichotokea tarehe 26/12/2015.

Shukrani za  dhati kwa Wachungaji wa kanisa la Umoja la  Chuo kikuu cha  Dsm kwa kuendesha ibada ya kumuaga Dr Chiduo na Kanisa la  Aglicana Magubike Kilosa Morogoro kwa kuendesha ibada ya mazishi. Madaktari, Wauguzi wa Hospitali ya Muhimbili na Marie Stopes Kwa Jitihada zao za kuokoa Maisha ya Dr Eliezer Chiduo.

Kwa namna ya Pekee familia inatoa shukrani za dhati kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki Wote,  Uongozi, Wafanyakazi na wanachuo wa Chuo kikuu cha Dsm,  BAKITA,  Manispaa ya  Kinondoni,  Bank M,   Majirani wa Chuo Kikuu   Cha Dsm,  Mbezi Msakuzi,  Kikundi cha maombi cha Ebenezer na  Wanakijiji wote wa Magubike  Kilosa  Morogoro  kwa huduma zote walizozitoa kipindi Cha Msiba.

Kwa vile si rahisi kuwataja wote kwa taarifa hii, Tunawaomba  wote mpokee Shukrani zetu za dhati kwa Moyo wa Upendo.

Shukrani yetu kubwa ni kwa Mungu Mwenyezi kwa kutupatia zawadi ya maisha ya Dr Chiduo hapa duniani na tutaishangili azawadi hii kwa kumsifu na kumtukuza Mungu siku zote za maisha yetu.

Tunapenda kuwakaribisha wote kwenye Misa ya Shukrani itakayofanyika Kanisa la Umoja (CCT Chaplains) Ukumbi  wa  Yombo Five(5) Chuo Kikuu Cha Dsm,  Jumapili ya Tarehe 07 February 2016   saa 1 :00 asubuhi.

“Kwa  maana sisi,  wenyeji wetu uko mbinguni;  kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi,  Bwana Yesu kristo; atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufananana mwili wake wa utukufu, kwa  uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha  vitu vyote viwe chini yake “Wafilipi 3:20-21

BWANA AMETOA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE APUMZIKE KWA AMANI...

AMINA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...