Chama
cha mapinduzi- Tawi la California, tunapenda kutoa salamu za pole zilizojaa
masikitiko makubwa kwa familia na ndugu wa Marehemu wa Mwenyekiti wa Tawi la
CCM la DMV Mzee George Sebo.
Pia tunapenda kutoa pole kwa uongozi wa chama wa
tawi la DMV kwa kuondokewa na kiongozi wao mahili. Lakini pia tunapenda kutoa
pole kwa watanzania wote wa DMV na wengine wote waliomjua marehemu.
Tumesikitishwa
na kuguswa sana na huu msiba hasa kwa kumjua marehemu kwa ukaribu sana, kwa
mapenzi yake kwa watu wote na nchi yake. Wengi wetu huku northern California
wanaccm na wasio wanaccm tunamjua marehemu kwa ukaribu kwani alikuwa
akitutembelea huku mara kwa mara na kuna kipindi yeye na mke wake walikuwa
wanachama wa jumuiya yetu ya watanzania waishio hapa bay area.
Hivyo ni mtu
wetu tunafahamu fika.
Kama
chama tutamkumbuka sana kwa kuwa mzee wa ushauri katika chama chetu na matawi
yetu hapa Marekani. Tutayazingatia yale yote aliyotuachia na kuyafanyia kazi.
Tunaomba
mungu wa rehema aiweke
roho yake mahala pema peponi.
AMINA
Erick Byorwango
Karibu-Tawi la California.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...