Wadau wa mazingira kutoka idara na wizara mbalimbali za serikali na mashirika binafsi wamekutana Januari 20, 2016 kujadili njia mahususi za kuboresha mazingira na kukabilaiana na athari za mabadiliko ya tabianchi kwenye majiji
Majadiliano hayo ni hatua moja wapo ya uanzishwaji wa mfuko wa Mfuko wa Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi ukiwa na lengo la kukusanya pesa za kukabiliana na changamoto za mazingira na mabadiliko ya tabianchi katika Manispaa ya Ilala
Mradi huo unafanywa kwa ushirikiano wa Manispaa ya ilala na ForumCC
Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu Rais, Ngosi Mwihava akifungua mkutano huo wa wadau ambao umewashirikisha pia watendaji wa serikali na mashirika yasiyo ya serikali kutoka katika wizara na idara mbalimbali, kwa lengo la kujadili kwa pamoja namna ya kushirikiana na kupata njia ya pamoja ya kuboresha mazingira na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi zikiwemo mafuriko, magonjwa na uharibifu wa miundombinu.
Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu Rais, Ngosi Mwihava (katikati) akiwa na viongozi wa Forumcc wakati wa mkutano huo, kuanzia kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia Mabadiliko ya Tabianchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Richard Muyungi, Mkurugenzi wa Mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Julius Ningu wakati kuanzia kulia ni Afisa Miradi Forumcc, Fazal Issa na Mwenyekiti wa bodi ya forumcc, Yusta Kibona
Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Dr. Julius Ningu akifafanua jambo wakati wamkutano huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...