Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kuutaarifu Umma wa Watanzania kuwa Uchaguzi wa Ubunge katika Jimbo la Kijitoupele – Zanzibar utafanyika mnamo tarehe 20 Machi, 2016.
Uchaguzi wa Mbunge katika Jimbo la Kijitoupele - Zanzibar ni mojawapo ya Majimbo yaliyoahirisha kufanya Uchaguzi tarehe 25 Oktoba, 2015 kutokana na hitilafu kwenye Karatasi za Kura.
Aidha, Tume inapenda kuwataarifu Wananchi kuwa Watendaji (Msimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi) walioteuliwa kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa 2015 ndio watakaosimamia na kufanya shughuli za Uchaguzi huo. Uchaguzi huo wa Ubunge katika Jimbo la Kijitoupele hautakuwa na Kampeni na Wagombea walioteuliwa kushiriki Uchaguzi ulioahirishwa mwezi Oktoba, 2015 ndio watakaoshiriki Uchaguzi huu.

Vituo vilivyotumika katika Uchaguzi wa mwaka 2015 ndiyo vitakavyotumika. Vituo vitafunguliwa saa 1.00 asubuhi na kufungwa saa 10.00 jioni. Watakaoruhusiwa Kupiga Kura tarehe 20/3/2016 ni wale ambao wameandikishwa na majina yao yapo katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura la Kituo na waje na Kadi ya Mpiga Kura.

Imetolewa na,
Jaji (Mst.) Damian Z. Lubuva
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
MWENYEKITI
26/01/2016

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...