Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bi. Amanda Fredrick Luhanga enzi za uhai wake.

AFISA Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bi. Amanda Fredrick Luhanga, amefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia Jumamosi Februari 27, 2016. Taarifa ya kifo cha Bi. Amanda imethibitishwa na Meneja Uhusiano wa TTCL, Bw. Nicodemus Thom Mushi.

 "...Ni kweli, Bi Amanda amefikwa na umauti akiwa likizoni mkoani Mbeya alikokwenda kuwasalimu ndugu zake.. Aliugua ghafla Alhamisi hii na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya hadi usiku wa kuamkia Jumamosi ambapo Mungu alimchukua," alisema Bw. Thom Mushi.

 Alifafanua kuwa mwili wa marehemu utasafirishwa siku ya Jumapili, kutoka Mbeya kwenda Njombe na Mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumatatu tar 29.02.2016 katika Kijiji cha Mlangali, Ludewa, Mkoa wa Njombe. Mtandao huu unatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Bi. Amanda Fredrick Luhanga kwa msiba mkubwa uliowafika.  Bwana alitoa, Bwana ametwaa, Apumzike kwa Amani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...