Kikosi cha timu ya soka ya Benki ya Exim Tanzania ambacho kiliibuka na ushindi wa mabao 1-0 dhidi ya Benki ya Akiba katika mechi ya robo fainali ya ligi ya mabenki iliyofanyika katika Viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Mkuu wa Hazina wa Benki ya Exim, George Shumbusho akimkabidhi zawadi winga wa timu ya Benki ya Exim Yussuf Abdillah, aliyefunga bao pekee lililoipeleka timu hiyo nusu fainali katika mechi ya robo fainali ya ligi ya mabenki iliyofanyika katika Viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Timu ya soka ya Benki ya Exim imetinga hatua ya nusu fainali ligi ya mabenki baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Benki ya KCB katika mchezo mkali uliofanyika katika Viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Ni winga Yussuf Abdillah wa Exim aliepeleka msiba kwa wapinzani wao baada ya kufanikiwa kuwazidi ujanja walinzi watatu wa timu ya KCB na kufanikiwa kufunga goli la pekee kwenye mchezo huo.
Ushindi huo umeiwezesha timu hiyo kutinga hatua ya nusu fainali ambapo itakutana na timu ya Benki ya DTB huku wachambuzi wa soka wakiipa nafasi zaidi timu ya Exim kutinga hatua ya fainali na hatimaye kujitwalia kikombe hicho muhimu katika nyanja ya michezo kwa timu za benki hapa nchini.
Wafanyakazi wa benki hizo na mamia ya mashabiki wa mpira walijitokeza uwanjani hapo kuzishangilia timu hizo katika mechi hiyo iliyotawaliwa na shangwe za mashabiki katika muda wa mchezo.
Ligi hiyo, inayoshirikisha benki zaidi ya 16, inalenga kuimarisha urafiki na ushirikiano baina ya mabenki licha ya kuwa washindani kibiashara.
Akizungumzia ushindi huo mara baada ya kuisha kwa mchezo Mkuu wa Hazina Benki hiyo Bw George Shumbusho ambaye pia ni mchezaji wa timu hiyo aliwapongeza wachezaji wenzie kwa uwezo mkubwa waliounyosha tangu mwanzo wa ligi hiyo huku akiahidi zawadi iwapo timu hiyo itafanikiwa kuchukua kikombe hicho.
“Shukrani za dhati ziwaendee wachezaji hususani mfungaji wetu wa bao pekee waliotoa muda wao na kuweka juhudi, ujuzi na nguvu zao ili kupata ushindi huu . Nawasihi wachezaji waendeleze juhudi hizi ili tuweze kuibuka washindi wa jumla katika mashindano haya,” alisema .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...