Katika Mkutano huo,Mwigulu pamoja na wananchi wamekubaliana tar 21/02/2016 kutafanyika mkutano mkubwa utakao husanisha wakulima na wafugaji ilikuweka mipaka ya kutenganisha eneo la kufigia na kilimo.
Wakati huohuo wote walioshiriki kwenye tukio la kukata kata mifugo wameshaanza kukatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria,Mwigulu amesisitiza kuwa si vyema kujenga tabia ya visasi baina ya wakulima na wafugaji.Serikali imeshajipanga kuanza kugawa maeneo kwaajili ya jamii hizi mbili katika sehemu mbalimbali za nchi,hivyo basi wananchi wa Mvomero na sehemu zingine wawe wavumilivu wakati huu serikali ikianza kugawa maeneo upya kwaajili ya hifadhi,kilimo na malisho ya mifugo.
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba akipokea baadhi ya maelezo kutoka kwa Mkuu wa polisi (RPC) Mkoa wa Morogoro kuhusiana na tukio la mapigano ya wakulima na wafugaji eneo la Mvomero.
Mama mjane akilia mbele ya mifugo yake iliyouawa kwa kukatwakatwa mapanga.
Hivi siku hizi raia wanaruhusiwa kuvaa mavazi ya kijeshi kama alivyofanya waziri nchemba?
ReplyDeleteKuua mifugo ya mjane mmemusa Muumba wake mboni ya jicho. Chavuyemo
ReplyDeleteSub'hanallah! Kweli inatilisha imani, pole sana Mama wa watu tena mjane, hata imani binaadam hatuna imetutoka kabisa! Pengine Mama huyo mjane alikuwa anajipatia rizki yake ya halali kupitia humo humo kwenye mifugo yake, leo hii mmekwenda kumcharangia kwa mapanga mifugo yake tena mizima mizima na kuiteketeza yote, analia maskini kwa uchungu na kufikiria mengi. Pole Mama mjane wa watu, Mwenyeez Mungu anashuhudia yote hayo na In Sha Allah atakulipia pia kukujaalia wepesi katika kutarazaki kwako licha ya kuwa wamekuangamizia kipato (mifugo yako). Tufike wakati jamani tukumbuke dunia ni ya kupita tu, tuuthamini utu tusitokwe imani kwa ajili ya vitu tu.
ReplyDelete