Afisa Wanyamapori Mkuu kutoka Wizara
ya Mali Asili na Utalii Bw. Pellage
Kauzeni akitoa wito kwa wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya ardhi oevu
kushirikiana na Serikali katika kuyatunza maeneo hayo. Kushoto ni Afisa
Wanyamapori kutoka Wizara ya Mali Asili na
Utalii Bw.Sadick Lotha na kulia ni Afisa Habari wa wizara hiyo Bw. Lusungu
Helela.
Afisa Wanyamapori kutoka Wizara ya Mali Asili na Utalii
Bw.Sadick Lotha akiwaeleza waandishi wa
habari leo jijini Dar es salaam kuhusu maadhimisho ya siku ya ardhi oevu
Duniani inayotarajiwa kufanyika februari 2,2016 ambapo siku hiyo itatumika
kutoa elimu kwa kuwakumbusha watu kuhusu uhifadhi na matumizi endelevu ya
rasilimali za ardhi oevu. Kulia ni Afisa Habari wa Wizara hiyo Bw. Lusungu
Helela, kushoto ni Afisa Wanyamapori Mkuu na Mratibu Kitaifa wa Uhifadhi Ardhi
Oevu Bw. Pellage Kauzeni.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...