Katibu Mkuu wa wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, wazee na watoto, Dkt. Ulisubisya Mpoki akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Siku ya saratani, huadhimishwa duniani kote kila mwaka ifikapo tarehe 4 ya Mwezi februari.
Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Saratani Duniani mwaka huu ni ‘TUNAWEZA, NINAWEZA. KWA PAMOJA TUWAJIBIKE KUPUNGUZA JANGA LA SARATANI DUNIANI.” (We can, I can. How everyone, as a collective or as an individual can do their part to reduce the global burden of cancer).

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Ocean Road, Julius Mwaiselage akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na huduma za matibabu zinazotolewa na Taasisi ya Ocean Road.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu Mkuu wa wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, wazee na watoto, Dkt. Ulisubisya Mpoki leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Taasisi ya Ocean Road pamoja na wadau mbalimbali kuadhimisha siku ya Saratani kuanzia kesho kwa kutoa elimu ya umuhimu wa kuzuia na kujikinga na madhara mbalimbali yatokanayo na maradhi ya Saratani ambayo hufanyika kila Februali 4 ya kila mwaka .
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Ulisubisya Mpoki amesema kuwa Saratani ni ugonjwa ambao unaathiri watu wa rika na jinsia zote; watoto, watu wazima, wake kwa waume.
Amesema takwimu za Shirika la Kimataifa la Atomiki la Utafiti wa Saratani (IARC) na Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaelezea kwamba kila mwaka duniani kunatokea wagonjwa wapya wa saratani wanaokadiriwa kufikia milioni 14.1, kati ya hao, zaidi ya wagonjwa milioni 8.2 hufariki dunia kutokana na ugonjwa wa Saratani, hii husababishwa kwa wagonjwa kuchelewa kufikishwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya. Vifo vya ugonjwa wa Saratani ni asilimia 13 ya vifo vyote vinavyotokea duniani (WHO).
Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Saratani duniani mwaka huu ni ‘‘Tunaweza , Ninaweza.Kwa pamoja tuwajibike kupunguza janga la saratani duniani’’.
Dk.Mpoki amesema kuwa hatua madhubuti za kinga, uchunguzi wa mapema na tiba stahiki hazitachukuliwa haraka, tatizo la Saratani litaongezeka na kufikia makadirio ya wagonjwa wapya milioni 24 ifikapo mwaka 2035, huku ongezeko kubwa likiwa katika ukanda wa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania.
Amesema tatizo la Saratani limekuwa likiongezeka na kukua, kila mwaka, Takribani wagonjwa wapya wapatao 44,000 hugundulika na saratani za aina mbalimbali nchini, hii ni sawa asilimia 10 tu (4,400) kati ya wagonjwa wote wanaofanikiwa kufika katika Taasisi ya Saratani Ocean Road ili kuweza kupata tiba. Kati ya hao wanaobahatika kufika katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (takribani asilimia 80) hufika wakiwa katika hatua za mwisho za ugonjwa (Hatua ya 3 na ya 4), hali ambayo hupunguza uwezekano wa wagonjwa kuweza kupona maradhi hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...