Mke wa Rais Mstaafu na Mwenyekiti wa WAMA akisalimiana na Mama Othman Chande alipowasili katika Shule ya Sekondari Tambaza kuhudhuriaWorld Thinking Day iliyoandaliwa na Tanzania Girl Guide Association.
Wanachama wa Girl Guide wakiwasili katika Shule ya Sekondari Tambaza katika kusherekea World Thinking Day ambao walipokelewa na Mgeni Rasmi Mama Salma Kikwete.
Picha ya Pamoja na Mgeni Rasmi na baadhi ya wanafunzi Wanachama na viongozi wa Girl Guide.
PICHA
NA YUSUPH BADI.
Na Philomena Marijani-
Meneja Uraghbishi na Mawasiliano, WAMA
CHAMA cha Girl Guide
Tanzania kimetakiwa kuweka mikakati ya kuhakikisha inaongeza wanachama
watakaojiunga na chama hicho ili vijana wengi waweze kunufaika.
Rai hiyo imetolewa
mwishoni wa wiki na Mke wa Rais Mstaafu na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mama Salma
Kikwete wakati wa maadhimisho ya kilele
cha siku ya World
Thinking Day yenye kauli mbiu ya Ungana, Shirikiana, Sherekea iliyoadhimishwa na Tanzania Girl Guides
Association. Sherehe hizo zilianza kwa maandamano ya wanafunzi Wanachama kutoka
Upanga katika Makao Makuu ya Girl Guide Tanzania na kumalizikia katika Shule ya Sekondari Tambaza ambapo sherehe rasmi ilifanyika hapo.
Akiongea katika sherehe
hizo Mama Salma Kikwete alipongeza
uongozi wa Girl Guide kwa kufikia mikoa
19 ambapo mpaka sasa chama kina wanachama 97,143 na aliongeza kuwa changamoto
kubwa waliyonayo ni kuongeza Wanachama zaidi kwani Tanzania ina watu wengi
sana.
“Wito wangu kwenu ni
kuongeza juhudi ya kuwafikia vijana wengi zaidi kwani sote tunajua umuhimu wa
TGGA katika kuwasaidia vijana kujiepusha na changamoto mbalimbali katika makuzi
yao. Ni lazima tuweke malengo ya muda mfupi, kati na mrefu ndani ya miaka
mitatu ili ifikapo mwaka 2018 tuwe tumeingiza
wanachama zaidi ya 100,000/= Tumieni vizuri shule za msingi na sekondari , nina
hakika mtafanikiwa kwa kiasi kikubwa sana. ” Alisema Mama Kikwete
Mama Kikwete pia
alishauri uongozi wa Girl Guide Tanzania kubuni mbinu
za kukabiliana na changamoto kwa kutumia rasilimali walizonazo.
“Kwa kuwa TGGA ni chama
kikongwe, chenye rasilimali kama ardhi ambazo ziko sehemu nzuri kibiashara naamini kwamba ikitayarishwa mipango mizuri mnaweza kupata wabia wenye tija au mkawekeza
kama chama kwa kushirikiana na mabenki. Mtakusanya kodi ambazo zitasaidia
uendeshaji na kuongeza uwekezaji. ”Alisema Mama Kikwete.
Akielezea maana ya
World Thinking Day Mkufunzi wa Taifa wa Tanzania Girl Guide Association, Mama
Magreth Olumbe alisema kuwa sherehe hii ilianza rasmi mwaka 1926 ambayo ni siku
ya; kuwakumbuka Girl Guide wote duniani na hasa wale walio kwenye mazingira
magumu;kuongelea mambo yanayowagusa wasichana kwa mfano mimba za utotoni,
kuolewa katika umri mdogo; na kukumbuka mwanzilishi wa Chama Lord Baden Powell
na mke wake Olave Baden Powell.
Akisoma risala kwa
Mgeni Rasmi, Kamishna Mkuu wa Tanzania Girl
Guides Association, Mama Symphorosa Hangi alisema kuwa katika kuadhimisha World
Thinking Day walikuwa na wiki mbili za kutoa huduma kwa jamii ikiwemo
kuwatembelea wagonjwa katika hospitali ya Ocean Road na kutoa chakula,
mavazi na nauli za kuwarudishwa makwao
wale waliokuwa wameruhusiwa baada ya matibabu. Aliongeza pia walitumia muda huo
kuhamasisha wasichana wengine kujiunga na chama cha Tanzania Girl Guides ili
nao waweze kupata fursa ya kujikwamua kifikra kwa kupitia mafunzo yanayotolewa
na chama.
Chama cha Girl Guides
Tanzania (TGGA) kilianzishwa hapa nchini mwaka 1928. TGGA ni chama kisicho cha
serikali na ni cha kujitolea chenye lengo la kuwaendeleza watoto wa kike na
wanawake kwa ujumla kushiriki katika maswala ya kijamii na kiuchumi kwa kupitia
elimu na mafunzo yanayotolewa kwa kuzingatia kanuni za Girl Guides pamoja na
kuwajenga kimaadili.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...