Alikiba anatarajiwa kuzindua wimbo wake mpya “lupela” siku ya alhamisi tarehe 4 februari 2016. Wimbo uliokuwa ukisubiriwa sana na mashabiki wake kutoka ndani na nje ya Afrika mashariki.

Video inayoonyesha wimbo huo ilishutiwa jijini Los Angeles, Marekani wakati ambapo Alikiba alialikwa kama mgeni rasmi katika tukio kubwa lililoandaliwa na Shirika la kimataifa la wanyama pori WildAid.

Chini ya kauli mbiu “Ujangili unatuumiza sote”, Alikiba amekuwa akifanya kazi sambamba na WildAid kuhamasisha wananchi Tanzania juu ya  hatma ya tembo wa taifa la Tanzania, ambao maelfu yao wamekuwa wakiuawa kikatili kwa ajili ya pembe zao.

“Ninafuraha kutoa wimbo mpya”, alisema Alikiba. “Lakini najivunia kwamba Lupela imewalenga zaidi tembo wa Tanzania, na natumaini mashabiki wangu wote watauona uhitaji mkubwa wa kuwalinda tembo wetu na kutokomeza biashara ya pembe za ndovu kama vile nionavyo mimi”
“Kampeni hii ni kitu muhimu sana kwa Alikiba na kwangu mimi pia kama meneja wake. Tutaendelea kufanya bidii na kutumia mbinu zote kusaidiana na WildAid kwenye kazi ya kulinda tembo wa Tanzania.” – Christine Mosha

Katika tukio nyota na la kusisimua litakalofanyika katika hoteli ya Slipway jijini Dar es salaam, wageni waalikwa na vyombo vya habari watapata fursa ya kuona video na kuusikiliza wimbo huo kwa mara ya kwanza.

“Tunajivunia kuwa na msanii Alikiba kama balozi wa WildAid”, alisema Salome Gasabile kutoka WildAid. “Kwa mwaka uliopita amekuwa akifanya kazi kwa bidii bila kuchoka kwa ajili ya tembo, na tunatumaini kwamba wimbo huu utaleta hamasa kubwa”

Tanzania imepoteza 60% ya tembo wake tangu mwaka 2009. Mamia ya tani za pembe za ndovu zimepenyezwa kinyemela kupelekwa nchini China na maeneo mengine.

Mwaka 2009 Tanzania kulikuwa na tembo takribani 110,000. Kufikia mwaka 2014, idadi ya tembo ilipungua kufikia 43,000.

Alikiba ana mpango wa kuachia filamu yake fupi kuhusu safari yake alipotembelea mbuga ya wanyama ya Tarangire, ambapo alitumia  muda wake kutizama tembo wakiwa mbugani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...