JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemteua Bwana Masanja Kungu Kadogosa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), ambako anakwenda kuchukua nafasi ya Mhandisi Elias Mshana ambaye anastaafu hivi karibuni.
Kabla ya Uteuzi huo Bwana Masanja Kadogosa alikuwa Mkurugenzi Idara ya Mikopo Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB). Uteuzi huo unaanza mara moja.
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
02 Februari, 2016.



Hivi iakuwaje mtu anateuliwa kukaimu nafasi!!?? Mimi nilidhani ukaimu ni ni automatic kutokutana na position yako. Mfano rais akiwa nje ya nchi, makamu anakaimu, then spika wa bunge and forth. Hata mkurugenzi mkuu ana msaidizi atakayekaimu in case of death,termination or suspension. I could be wrong naomba nielimishwe
ReplyDeleteKukaimu hapo ina maana ya "interim", kwamba ni uteuzi wa muda, baadaye atafanya permanent appointment ya full term.
ReplyDeleteMdau no.1 uko sahihi kabisa. Kukaimu ni kushika nafasi/ wadhifa kwa muda, mpaka hapo anaetakiwa kuchukua nafasi hiyo atakapopatikana au atakaporudi kwenye nafasi yake. Kwa TRL, management yote ni uozo mtupu, hata wa kukaimu hiyo nafasi hamna bora apelekwe huyo wa muda akutane na changamoto na tunaamini atazitatua, tena na hiyo management yenyewe ingefaa kama ingekaa pembeni kabisa. Uwezo wao wa kufikiri umeshafikia ukingono ndo maana madudu ni mengi ndani ya kampuni hiyo
ReplyDelete